Shabiki afariki baada ya Penalty kati ya Chile na Brazil.


chilee
Shabiki mmoja wa mpira wa miguu aliyekuwa nchini Brazil wakati mechi kati ya Brazil na Chile ikichezwa amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati wa kipindi cha makabiliano ya penalty.Shabiki huyo alikua akiangalia mpira kwenye moja ya Baa iliyopo ndani ya Mineirao ambapo baada ya Penalty hiyo alianza kulalamika kuwa hajisikii vizuri na kupelekwa hospitali ambako baadae alipoteza maisha.Kwa mujibu wa Gazeti la Estado de minas shabiki huyo alikua miongoni mwa watu 98 waliokuwa wakipatiwa huduma ya kwanza kutoka kwa wahudumu wa afya waliokuwa ndani ya eneo lililokuwa na takribani watu 60 waliokuwa wakihudumiwa kwenye viti vyao.

chilee2
Mechi hiyo iliishia kwa sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida na kupelekea kuchezwa kwa muda wa ziada ambao haukuzalisha chochote.
Wakati wa matuta timu ya Brazil ilipoteza mara mbili sawa na Chile jambo lililochangia taharuki miongoni mwa Mashabiki wa timu ya nyumbani ya Brazil.
Baadaye aliyekuwa mchezaji wa West Brom Gonzalo Jara wa Chile aligonga mwamba hivyo kuwapa Brazil nafasi ya kuingia robo fainali.
Mwanaume huyo aliyekufa eneo la kuangalia mpira si wa kwanza kwenye mechi ya kombe la dunia ambapo China mtu mmoja alikufa baada ya kukaa macho siku tatu kushuhudia mechi ya ufunguzi kwenye makundi, ambapo shabiki wa Mexico alijirusha na kufa baada ya timu yake kusajili ushindi kwenye mechi ya ufunguzi
Previous
Next Post »