TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 11.06.2014.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI.
·
MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
·
WAPIGA DEBE 09 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIFANYA FUJO MAENEO YA STENDI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WOLTER
JONATHAN (36) MKAZI WA MOROGORO
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.06.2014 MAJIRA
YA SAA 04:30 JIONI KATIKA BARABARA
KUU YA MBEYA/NJOMBE KATIKA KIJIJI CHA MBUYUNI, KATA YA MAPOGORO, TARAFA YA
RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO,
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
SERIKALI MBARALI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA
DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI IDUDA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LEUS JOHN (07) MKAZI WA IDUDA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.06.2014
MAJIRA YA SAA 20:40 USIKU KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU ENEO LA UYOLE - MAGOROFANI, KATA YA IGAWILO,
TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASAJILE
MWAKISAMBWE (41) MKAZI WA KIJIJI
CHA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 52.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.06.2014
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KITONGOJI
CHA MAJENGO, KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WAPIGA DEBE 09 WANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO MAENEO YA STENDI YA MABASI
ILOMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA KUFUATI MGOMO WA DALADALA.
WATUHUMIWA HAO
NI PAMOJA NA 1. IPYANA MWANGOMOLE
(27) MKAZI WA MAKUNGULU 2. HUSSEIN
HASSAN (32) MKAZI WA ILEMI 3.
ZAKARIA LIANDA (23) MKAZI WA AIRPORT 4.
BAHATI MATHIAS (28) MKAZI WA SAE 5. BONIFACE
JASSON (22) MKAZI WA ITUHA 6. AMOS
ROBERT (16) MKAZI WA SAE 7. OTTO
JEKI (21) MKAZI WA ILOMBA 8. ALEX
MWAIKUJI (28) MKAZI WA AIRPORT NA 9.
LEOFASI ANTHONY (17) MKAZI WA
SAE. WATUHUMIWA WALIKUWA WAKIWA WANAFANYA FUJO KUFUATIA MGOMO WA DALADALA.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.06.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA
STENDI YA MABASI ILOMBA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA.
TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYWA.
Imetolewa na:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon