Mswada wa kuuza Mwili wa Marehemu kwa Serikali ili utumike kwa Utafiti wazua kashehe Kenya

Changamoto ya upatikanaji wa maiti za kufanyia tafiti mbalimbali za kiafya nchini Kenya imeilazimu serikali ya nchi hiyo kupeleka bungeni mswada wa sheria ya afya utakaorahisisha upatikanaji wa maiti katika sekta ya afya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na kituo cha runinga cha Citizen cha Kenya, Wizara ya Afya ya Kenya imeeleza kuwa kadri wanafunzi wa udaktari wanavyoongozeka na magonjwa ya aina mbalimbali yanayoripuka ndivyo changamoto katika utafiti hasa upatikaji wa maiti inavyoongozeka.
Kwa kuzingatia hilo, wizara hiyo imeamua kupeleka mswada bungeni unaoeleza kuwa endapo mtu atafiki bila kuacha wosia mwili wake ufanyweje baada ya kufariki, basi ndugu wa mtu huyo wakiongozwa na mkewe/mmewe wanaweza kuridhia kuutoa mwili huo kwa ajili ya utafiti serikalini.
Hata hivyo, wizara ya afya imeeleza kuwa wanapata maiti wengi ambao hawatambuliki na ndugu zao lakini wanakuwa hawawezi tena kutumika kwa kuwa utafiti huhitaji maiti ambao hawajakaa muda mrefu.
Mswada huo umegeuka changamoto kubwa kwa watu mbalimbali nchini humo kwa kuwa suala la mwili wa marehemu kwa wengine ni ibada.
Hata hivyo hofu kubwa ya mswada huo ni pale ambapo litatangazwa donge nono kwa wale watakaopeleka miili ya marehemu kuwa huenda watu wakafanya hila kujipatia pesa.
“Kwa mwili wa mtoto ndio nasema milioni moja, ikiwa ya mtu mzima iwe kama milioni mbili na nusu hivi.” Alisema raia mmoja aliyehojiwa.
Aidha, serikali hiyo imetoa angalizo kwa wale watakaotumia madaktari kutoa viungo vya mwili wa marehemu kujipatia pesa kinyume cha hatia kuwa watakumbwa na hatia na kuuona mkono wa sheria.
Isikilize habari hii hapa:
Previous
Next Post »