
Yusta Lucas akionyesha makovu yake ya mgongoni ambayo aliyapata kwa kung'atwa na kuchomwa na pasi na mwajili wake. Picha na Esther Kabakaya

Sehemu ya majeraha kwenye mwili wa binti aliyejeruhiwa na mwajiri wake
------
Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho. Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.
Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi ndogondogo.”
Alisema aliishi vizuri na mwajiri wake huyo, lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa akinichapa na kuning’ata sehemu mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma kwa pasi yenye moto kila aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.............
EmoticonEmoticon