Mahakama moja nchi Misri imemtia hatiani dereva mmoja wa Taxi na kumpiga faini ya paundi 5,000 za nchi hiyo ni sawa na Sh. Milioni moja ya Tanzania, baada ya kumwita mwanamke demu.
Dereva huyo alikumbwa na mkasa huo wakati akiwa katika mishemishe zake za kawaida ndipo alipokutana na maandamano ya wanawake wanaopinga kitendo cha kubakwa mwanamke mweziwao na kundi la vijana wiki mbili zilizopita katika uwanja wa mapinduzi jijini Cairo.
Dereva huyo akiwa ndani ya gari yake alikutana na wanawake hao na kumwambia mwanamke mmoja aliyekuwa mbele yake wasaa ya muza (pisha wewe demu) kauli ambayo imetafsiriwa kuwa ni ya unyanyasaji wa kijinsia.
EmoticonEmoticon