KIJANA AFARIKI DUNIA HAPO HAPO BAADA YA KUANGUKIW NA KICHUGUU.SAMAHANI PICHA NI MBAYA


Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera Raulian Ladislaus mwenye umri wa Miaka 40, ukiwa umeangukiwa na Kichuguu na kufariki papo hapo June 12,2014,mchana wakati akichimba kichuguu hicho kwa lengo la kuangamiza mchwa waliokuwa wakiharibu miwa yake aliyoilima karibu kichuguu hicho.




Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 asubuhi wakati Marehemu akichimba kichuguu hicho ili kukihamisha kwa lengo la kusalimisha ekari moja ya Miwa iliyokuwa karibu na kichuguu hicho kabla ya kuangukiwa na kukandamizwa na Kichuguu hicho kifuani.
 
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Uganzo walishirikiana kuchimba kichuguu hicho kwa lengo la kumtoa marehemu ambaye alizikwa juzi June 12, 2014,Jioni Nyumbani Kwake.
Previous
Next Post »