GARI LA MILEY CYRUS LAPATIKANA





Gari la muimbaji Miley Cyrus lililoibiwa baada ya majambazi kuvamia nyumba yake ya Los Angeles limepatikana.
Kwa mujibu wa TMZ kuna mtu aliliona gari hilo lenye thamani ya milioni 218 likiwa limeegeshwa mtaani na kuwapigia simu maaskari. Inasemekana gari hilo halijaharibika na inahisiwa huenda majambazi waliogopa na kuamua kulitelekezwa baada ya kuona habari zimesambaa za kuibiwa kwake.
Miley Cyrus alikuwa nchini Sweden kwenye ziara ya Bangerz wakati majambazi wanavamia nyumba yake.
Previous
Next Post »