Wazee wa Mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi wakiambatana na viongozi wa mbalimbali wa dini kutoka katika maeneo hayo wakiwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere (JKNI) leo baada ya kuwasili nchini kwa shirika la ndege la Qatar, wakitokea nchini Thailand kujifunza shughuli mbalimbali za nishati ya gesi.
Baadhi ya viongozi wa dini kutoka katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand. Viongozi hao walifanya ziara nchini humo kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu wa uendelezaji wa sekta ya gesi.Baadhi ya viongozi wa dini wakiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand.
Viongozi wa dini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand.Padri Dkt. Aidan Msafiri ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino tawi la Mtwara akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Thailand.
Shehe Mkuu kutoka Mkoa wa Mtwara Bw. Nurdin Abdalah akiwaeleza waandishi wa habari jinsi wananchi wa Thailand walivyoweza kutunza vyema rasilimali yao ya gesi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa sekta nyingine.Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Hamis Ulega akizungumza na waandishi wa habari jinsi wananchi wa Thailand walivyonufaika na rasilimali ya gesi
EmoticonEmoticon