TAARIFA YA JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.05.2014.
Ø
WATU WATATU WAUAWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI
MKOANI MBEYA.
Ø
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI NA WENGINE WATATU
KUJERUHIWA.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA
TUHUMA ZA KUPIGA RAMLI CHONGANISHI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA
KUKUTWA NA BHANGI
TUKIO
LA KWANZA.
MTU
MMOJA JOSEPH ADMIN [35] MKAZI WA
KIJIJI CHA MATUNDASI WILAYA YA CHUNYA ALIUAWA
KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO,MAWE NA MARUNGU.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 15.05.2014
MAJIRA YA SAA 22:00HRS USIKU KATIKA
OFISI YA KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA
MATUNDASI TARAFA YA KIWANJA WILAYA
YA CHUNYA.
KUNDI HILO LA WANANCHI WAKIONGOZWA NA FABIANI JOHN NA THOBIAS ASUKENYE WALIVUNJA
MLANGO WA OFISI HIYO NA KUANZA KUMSHAMBULIA MAREHEMU AMBAYE ALIKUWA AMEKAMATWA
PAMOJA NA MWENZAKE ABBAS JUMANNE [29]
KWA TUHUMA ZA KUIBA VING’AMUZI VIWILI VYA STAR TIMES CHUNYA MJINI AMBAVYO
WALIKUTWA NAVYO. HATA HIVYO POLISI WALIFIKA ENEO HILO MARA BAADA YA KUPATA
TAARIFA ZA VURUGU HIZO NA KUFANIKIWA KUMUOKOA MTUHUMIWA ABBAS JUMANNE. WATUHUMIWA FABIAN JOHN NA THOMAS ASUKENYE WALIKIMBIA
WAO NA WENZAO WENGINE WALIOSHIRIKI KATIKA MAUAJI HAYO WANATAFUTWA WAKAMATWE
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE. LAKINI PIA WATU WENYE TABIA YA KUFANYA UHALIFU WAACHE KWANI
ITAPUNGUZA UWEZEKANO WA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WANAOJICHUKULIA SHERIA
MIKONONI.
TUKIO
LA PILI.
MTU
MMOJA FRED MWAKIBINGA [55], MKAZI WA
KIJIJI CHA KANGA – IPINDA WILAYA
YA KYELA ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI
KUPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUSHAMBULIWA
KWA KUPIGWA NGUMI NA MATEKE MWILINI NA KARUME
SOKONI [35], MKAZI WA KIJIJI CHA KANGA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014
MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA, KATA YA IPINDA,TARAFA YA NTEBELA WILAYA YA KYELA. CHANZO
CHA TUKIO NI UGOMVI ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA BAADA YA MTUHUMIWA
KUFUNGA NG’OMBE WAKE KWENYE SHAMBA LA MAREHEMU BILA IDHINI YAKE NA MAREHEMU
KUTAKA KUZITOA NG’OMBE HIZO SIKU YA
TAREHE 11.05.2014 MAJIRA
YA SAA 12:00HRS, HIVYO MAREHEMU ALIENDELEA KUPATA MATIBABU AKIWA NYUMBANI
HADI HALI ILIPOBADILIKA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA
MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.AIDHA ANATOA RAI
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
TUKIO
LA TATU.
MTU
MMOJA LACKSON KAHAWA MWASHIBANDA [66],MKAZI
WA KIJIJI CHA MASOKO-ISANGATI ALIUAWA KWA KUKATWA JEMBE KICHWANI NA FARAO ADAMU [27], MKAZI WA KIJIJI CHA
MASOKO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 15.05.2014
MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MASOKO, TARAFA YA ISANGATI,WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. MAREHEMU ALIVAMIWA
NJIANI NA MTUHUMIWA WAKATI AKIWA
ANAELEKEA SHAMBANI NA JEMBE LAKE KISHA KUMNYAG’ANYA JEMBE HILO NA KUMKATA NALO
KICHWANI. MTUHUMIWA AMBAYE ANAMATATIZO
YA AKILI AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA
KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA UANGALIZI MAALUM KWA WATU WENYE
MATATIZO YA AKILI WANAOISHA NAO ILI
KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
TUKIO
LA NNE.
WATU WAWILI REHEMA MWAMASO
[30],MKAZI WA SUMBAWANGA NA MWANAUME
MMOJA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,UMRI KATI YA MIAKA
30-40, WALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA WAKIWA KATIKA GARI
T.620 CTL AINA YA TOYOTA L/CRUISER PRADO
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ROBERT
JUBERY MWAIHOJE [61],MKAZI WA SUMBAWANGA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 15.05.2014
MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA NAKAWALE,TARAFA YA NDALAMBO,WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA YA SUMBAWANGA/TUNDUMA. KATIKA TUKIO HILO WATU
WENGINE WATATU WALIJERUHIWA AKIWEMO
DEREVA WA GARI HILO NA WANAWAKE WAWILI
AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA NA
MAKAZI YAO. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO
KASI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI DEREVA AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOYUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUFIKA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA
AJILI YA UTAMBUZI WA MAREHEMU NA
MAJERUHI.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO [05] KUTOKANA NA
MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA
TUKIO LA KWANZA JESHI
LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA KOSA LA KUPIGA RAMLI
CHONGANISHI. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
15.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00HRS MCHANA
HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA YA
MATWIGA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NI 1. TONNY
ERNEST @ KALAMATA [32], MKAZI WA MKOANI TABORA 2. SHABAN
RASHID [31], MKAZI WA MKOANI TABORA 3. BAILOS ISMAIL [31] MKAZI WA DSM PAMOJA NA MWENYEJI WAO EMANUEL KABUKA [30],MWENYEKITI WA KIJIJI HICHO AMBAYE PIA NDIYE
ALIYEWALETA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA NA KUACHA TABIA
YA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA
KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA IKIWA NI
PAMOJA NA KUSABABISHA MATUKIO YA MAUAJI NA
KURUDISHA NYUMA MAENDELEO KATIKA JAMII. NA YEYOTE ATAYEBAIANIKA KUFANYA VITENDO
HIVI POLISI HAITASITA KUWAKAMATA NA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI
YAKE.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA
MTU MMOJA ASWILE ANDONGWISYE [24]
MKAZI WA NKUYU WILAYA YA KYELA KWA KUKUTWA BHANGI KETE 64 ZENYE UZITO WA GRAM
320.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 15.05.2014
MAJIRA YA SAA 14:30HRS MCHANA HUKO KATIKA
ENEO LA NKUYU, KATA YA NKUYU, TARAFA YA
UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA,MKOA
WA MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AMBAYE NI MTUMIAJI NA
MUUZAJI WA BHANGI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon