Ampiga binti yake wa kambo na kumsababishia upofu wa maisha, kisa alifikiri anatoka na 'kijana wa kiislamu'



Ubaguzi wa aina yoyote ni vyema ukapigwa vita mapema kwa kuwa madhara yake ni makubwa kuanzia ngazi ya familia.
Mwanamke mmoja alitajwa kwa jina la Jageer Mirgind wa Uingereza, amepigwa vibaya na kusababishiwa upofu na baba yake wa kambo baada ya kuhisi kuwa ana uhusiano wa mapenzi na kijana wa imani ya kiislamu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Jageer kuhusu tukio hilo yaliyosomwa katika mahakama moja nchini Uingereza, baba yake huyo wa kambo aliyetambulika kwa jina la Manjt Mirgind mwenye umri wa miaka 51 alimvamia na kumburuza hadi jikoni huku akimtishia maisha ‘nitakuua’.
Wakati mzee huyo akitekeleza tukio hilo la kinyama, alikuwepo mtoto wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita ambaye alishuhudia akilia kwa sauti huku akijaribu kumvuta ili asiendelee kumtesa Jageer. Hata hivyo msaada wake haukuwekana. Mzee aliingiza vidole machoni mwa binti yake huyo na kumtoboa macho.
 Mtandao wa Dailymail umeripoti kuwa mzee huyo alichanganywa na simu zilizokuwa zinapigwa kwa watu kwa lengo la kuwatania (prank calls) ili kurusha kwenye vipindi kama sehemu ya show.
Baada ya kusomewa mashitaka yote na kukiri kosa mahakamani, mzee huyo alijitetea kupitia maelezo yaliyosomwa na mwanasheria wake.
“Mimi ni baba wa familia anaefanya kazi kwa bidii ambaye aliacha kazi ili amuangalie/amtunze mama yake aliyekuwa mgonjwa miaka saba iliyopita. Nilikuwa na msogo wa mawazo wakati huo na hakuna kinachoweza kuwa kisingizio kwa kile nilichofanya. Nilikuwa najaribu kumtetea binti yangu. Mimi ni mwanaume ninaependa amani na mwaminifu na najua sitakuwa na nafasi ya kuomba radhi lakini naitumia mahakama kiasi gani naomba radh
Previous
Next Post »