Ø
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO
LA KWANZA.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI
KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA KITWANA
S/O LUGOYA [30]
MKAZI WA ILEMI-JUHUDI ALIUAWA KWA
KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE,
FIMBO NA MARUNGU. CHANZO NI TUHUMA ZA UNYANG’ANYI/KUTEKA GARI. AWALI TAREHE 12.05.2014 MAJIRA YA SAA 02:30HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHANGAMWELU,
KATA YA MSHEWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI MKOA WA MBEYA. STEPHEN S/O MGOGO
[40] MKAZI WA KABALE AKIWA NA
WENZAKE KWENYE GARI AINA YA FUSO
WALIKUTA MAWE YAMEPANGWA BARABARA YA MBALIZI/MKWAJUNI NA DEREVA ALIPOSHUKA ILI KUTOA MAWE HAYO LILITOKEA KUNDI LA WATU WANNE KUTOKA VICHAKANI WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA NA MARUNGU
WALIWAVAMIA NA KUWASHAMBULIA KISHA KUWAPORA PESA, SIMU ZA MKONONI NA PIKIPIKI
MOJA T.682 CHT AINA YA SANYA ILIYOKUWA
NDANI YA GARI HILO NA KUTOWEKA KUSIKOJULIKANA. THAMANI HALISI
YA MALI ILIYOPORWA BADO KUJULIKANA. KUFUATIA
MSAKO ULIOFANYWA PIKIPIKI IMEPATIKANA NA
WATUHUMIWA WAWILI 1. NDAYOBI S/O LUTEGO
[26] MKAZI WA IGUNGA-TABORA
NA 2. IDDI S/O SADICK [29] MKAZI
WA VETA WAMEKAMATWA. MHANGA STEPHEN S/O MGOGO
AMELAZWA HOSPITALI TEULE YA IFISI HALI
YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI
WANAPOWAKAMATA WATUHUMIWA KWA TUHUMA MBALIMBALI BADALA YAKE WAHAKIKISHE
WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ICHUKULIWE. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. PIA
KAMADA MSANGI ANATOA RAI KWA JAMII HUSUSANI WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA WA
MAZAO KUEPUKA TABIA YA KUTEMBEA/KUWEKA
NDANI YA NYUMBA KIASI
KIKUBWA CHA FEDHA ILI KUEPUKA MATATIZO
YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI KATIKA TUKIO HILO JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42] MKAZI WA
KIJIJI CHA MKWANGU NA MAJIGITA S/O MUSSA [40] MKAZI WA UVINZA MKOANI
KIGOMA BAADA YA
KUKAMATWA WAKIWA NA NYARA ZA
SERIKALI NYAMA YA MNYAMA INSHA YENYE
UZITO WA KILO 3 PAMOJA NA NGOZI YA
KICHWANI YA MNYAMA HUYO.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA TAREHE 12.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISUNGU-MKWANGU, KATA
YA MAMBA,TARAFA YA KIWANJA WATUHUMIWA NI MTUMIAJI NI WAWINDAJI
HARAMU NA TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYWA ILI KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
NAYORAMU S/O WAJEKAJE [42] MKAZI WA
KIJIJI CHA MKWANGU WILAYA YA CHUNYA
BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAMU 500.
MTUHUMIWA
HUYO ALIKAMATWA TAREHE 12.05.2014
MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MKWANGU, KATA YA MAMBA,TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA.
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
KUMFIKISHA MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE
WAFUATE TARATIBU ZILIZOPO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI.
Imetolelewa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon