TAARIFA YA JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 05.05.2014.
·
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IYALA
AMEKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI YA BARABARANI WILAYANI MBARALI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA MWANANYELA KALIMANZILA (43) MKAZI WA KIJIJI CHA IYALA ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU
ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
04.05.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA IYALA, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA.
INAELEZWA KUWA MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE TANGU TAREHE 03.05.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI AKIWA NA MTOTO WAKE
WAKIELEKEA SHAMBANI UMBALI WA KILOMITA 170, WAKIWA SHAMBANI NDIPO ALITOKEA MTU
ALIKUWA AMEJIFUNGA MATAMBALA USONI NA KISHA KUANZA KUMKATA MAPANGA. CHANZO CHA
TUKIO HILI NI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA. MUME WA MAREHEMU ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA KALIMANZILA MAGOFI (70) ANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANA ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILI KWANI INADAIWA
KUWA ALIKUWA AKIMTUHUMU MKEWE KUWA ANAMROGA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATU WENGINE
WALIOHUSIKA ZINAENDELEA. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA BROWN MOGA (80) MKAZI WA KIGOE AMEFARIKI DUNIA
PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA
DEREVA WAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KIGOE, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO
KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA
BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBEA
MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI KUEPUKA AJALI .AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA
MSAKO:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA MADIBA BUHEMBO @ CHEREHANI (42) MKAZI WA KIMBEREKETE-MAPUGORO
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI
LENYE UKUBWA WA ROBO HEKTA.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
04.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA KIMBEREKETE, KIJIJI CHA MAPUGORO, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. BHANGI HIYO
INA UREFU WA FUTI SABA [07]. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KULIMA ZAO HARAMU LA BHANGI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA KILIMO CHA MAZAO MENGINE
YA CHAKULA/BIASHARA.
Imesainiwa
na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon