TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.05.2014.
MTU MMOJA AUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI
Ø
MOTO
WATEKETEZA SEBULE NA VITU VILIVYOMO
TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI
MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL RAYMOND DAUD [26], ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA
KUKATWA PANGA KICHWANI, SHINGONI NA KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 18.05.2014 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO
KIJIJI CHA KALUNGU KATA YA IVUNA TARAFA YA KAMASAMBA WILAYA YA MOMBA MKOANI
MBEYA. KANDO YA MWILI WA MAREHEMU KULIKUTWA DEBE LA UFUTA NA PANGA. CHANZO CHA
MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
.Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI PINDI WANAPOWAKAMATA WATUHUMIWA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE KWENYE
TAARIFA JUU YA ALIOHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WATUHUMIWA WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
TUKIO LA PILI:
MOTO WATEKETEZA SEBULE NA VITU VILIVYOMO
JACOB MWALEPEPO [64], ALIGUNDUA
KUNGUA MOTO KWA SEBULE YA NYUMBA
YAKE YENYE VYUMBA VIWILI NA SEBULE NA
KUTEKETEZA VITU MBALIMBALI
VILIVYOKUWA SEBULENI HAPO AMBAVYO THAMANI YAKE BADO KUFAHAMIKA TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 18.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS HUKO MTAA WA
SINDE “B”, KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. MOTO HUO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA
MOTO NA UOKOAJI, JESHI LA POLISI NA WANANCHI, KATIKA TUKIO HILO HAKUNA MADHARA
YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO KINACHUNGUZWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
.Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA VYUMBA ZETU ILI KUWEZA KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Imesainiwa na:
[ AHMED .Z. MSANGI -- SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon