HII NDIO NDOA YA AJABU NA YA AINA YAKE KUWAHI KUTOKEA TANZANIA.




Bibi na bwana harusi wakiwa wenye nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa. Bi harusi huyo anaitwa Maria Omar (25) baada ya kubatizwa siku hiyohiyo ya ndoa. Awali aliitwa Jamini. Bwana harusi anaitwa Adrian Octavian (53). Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa lililopo kwenye Kituo cha Kulea Wasiojiweza cha Amani kilichopo Chamwino, mjini hapa na mfungishaji alikuwa mtumishi wa Mungu, Padri Beatus Sewando. HISTORIA YA BI HARUSI Habari zilizowazi zinaonesha kuwa, bi harusi huyo amekulia katika kituo hicho ambacho hulea watu wenye matatizo mbalimbali, wakiwemo wenye mtindio wa ubongo kama alivyo bi harusi huyo. Alipelekwa kwenye kituo hicho akiwa na miaka sita baada ya wazazi wake kujiridhisha kwamba alikuwa mgonjwa wa akili.

UME MUHAMMAD (S.A.W) Padri huyo aliendelea kusema: “Nawasihi tufuate mafundisho ya Bwana Yesu na Mtume Muhammad (S.A.W) kuwasaidia ndugu zetu wenye matatizo mbalimbali. “Bwana harusi amefaulu jambo hilo kwani licha ya yeye kuwa na matatizo kidogo ya akili lakini ameamua kumuoa Jamini ambaye muda mfupi ujao atabatizwa na kupewa jina jipya la Maria. “Mimi ni Mkurugenzi wa Kituo cha Amani, Jamini tumemlea zaidi ya miaka nane sasa, tunamjua ana matatizo ya akili lakini hivyo bwana harusi ameamua kufunga naye ndoa na kubeba msalaba huo wa kumtunza mkewe siku zote za maisha yao. Haya ndiyo mafundisho ya Yesu na Mtume Muhammad.” BI HARUSI AHOJIWA, AJIBU NDIVYO SIVYO Baada ya ndoa hiyo, mwandishi wetu alimuuliza bi harusi anasemaje kuhusu tukio hilo la kufunga ndoa, lakini akachanganya mtazamo, msikie: ”Mtujengee nyumba (bila kumtaja nani ajenge), pale tunapokaa baadhi ya wapangaji wenzetu wanatuchokoza.”

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng