Didier Claude Deschamps austaajabisha ulimwengu kwa kumuacha Samir Nasri na Gael Clichy


Licha ya kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji walioipa ubingwa klabu ya Man City huko nchini Uingereza katika msimu wa mwaka 2013-14 uliofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita, kiungo Samir Nasri pamoja na beki wa pembeni Gael Clichy wameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kitaaanza kujiandaa na fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Kuachwa kwa kiungo Samir Nasri kumehusishwa na sakata la utovu wa nidhamu ambalo lilijitokeza wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, hali ambayo ilisababisha timu ya taifa ya Ufaransa kushindwa kuonyesha uwezo wake na kuondolewa kwenye hatua ya makundi.
Tukio hilo lilimuweka Samir Nasri pamoja na wachezaji wengine wa timu ya taifa ya Ufararansa kwa wakati huo katika mazingira magumu, halia mbayo ilisababisha wafungiwe kuichezea timu ya taifa kwa michezo kadhaa na shirikisho la soka nchini humo.
Samir Nasri, alikumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ambayo iliihusisha timu ya taifa ya Ufaransa, lakini baada ya hapo alirejeshwa kikosini na alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2012, zilizochezwa nchini Ukraine pamoja na Poland.
Kwa upande wa Gael Clichy ametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, kutokana na ushiriki wake hafifu kwenye kikosi cha klabu ya Man City, ikilinganishwa na wachezaji wengine waliotajwa katika nafasi ya ulinzi watakaokwenda nchini Brazil.
Wakati wachezaji hao wakiachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, wachezaji wengine tisa wanaocheza ligi ya nchini Uingereza wamejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambayo ipo chini ya kiungo na nahodha wa zamani wa timu hiyo Didier Claude Deschamps.
Kikosi cha wachezaji 23 kinachounda timu ya taifa ya Ufaransa tayari kwa fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil upande wa makipa yupo Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Mickael Landreau (Bastia).
Mabeki: Mathieu Debuchy (Newcastle), Lucas Digne (Paris St-Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny, Bacary Sagna (both Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid).
Viungo: Yohan Cabaye, Blaise Matuidi (both Paris St-Germain), Clement Grenier (Lyon), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille).
Washambuliaji: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (QPR - on loan at Newcastle), Franck Ribery (Bayern Munich), Stephane Ruffier (Monaco).
Wachezaji watakaosubiri endapo patatokea hitilafu yoyote kwenye kikosi cha wachezaji 23 kilichotajwa ni: Loic Perrin (St Etienne), Maxime Gonalons, Alexandre Lacazette (both Lyon), Morgan Schneiderlin (Southampton), Benoit Tremoulinas (Dynamo Kiev), Remy Cabella (Montpellier)

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng