Video: Hillary Clinton ashambuliwa na 'kiatu' wakati akihutubia Las Vegas


Hillary Clinton, aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani alijikuta katika wakati mgumu jana (April 10) baada ya kurushiwa kiatu na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikujulikana kwa haraka wakati akihutubia Las Vegas.
Bi. Clinton alikuwa akihutubia katika eneo la Mandalay Bay ambapo mwanamke huyo alirusha kiatu ghafla kwa lengo la kumpiga.
Hata hivyo, Clinton alikikwepa kwa ustadi kiatu hicho na kisha kuendelea na maelezo ya utani juu ya tukio hilo.Walinzi walimshika mwanamke huyo na kwenda nae nje na kwa mujibu wa Daily Mail alitupwa selo.
Tukio hilo linafanana na lile la George Bush kurushiwa viatu viwili na mwandishi wa habari alipokuwa akihutubia nchini Iraq mwaka 2008 na alivikwepa viatu vyote viwili.

Previous
Next Post »