TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 22.04.2014.






·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA SILAHA KINYUME CHA SHERIA

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILI WATU WANNE WAKIWA NA BHANGI.

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. HARUNA HALIDI (57) MKAZI WA MWAKAGANDA  NA 2. LAURENCE GOHAGI (55) MKAZI WA MADIBIRA WAKIWA NA SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE BILA KIBALI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KINYASUGUNYE, KATA YA MADIBIRA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI MNAMO TAREHE 21.04.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU. TARATIBU ZA KUWAFIKSHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIMILIKISHA SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA KUMILIKI SILAHA. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KNYUME CHA SHERIA AZITOE ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.




KATIKA MSAKO WA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE 1. STEPHEN JUMA (22) MKAZI WA MTAA WA MWAKA 2. ERICK KITWIKE (28) MKAZI WA MTAA WA MAJENGO 3. EPHRAIM ISAYA (24) MKAZI WA MTAA WA MWAKA NA 4. LUSAJO ADAM (21) MKAZI WA MTAA WA MWAKA WAKIWA  NA  BHANGI KETE 41 SAWA NA UZITO WA GRAM 205.

WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA HUKO KATIKA ENEO LA STENDI YA MABASI TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,   MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 21.04.2014 MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI BAADA YA KUFANYIKA MSAKO MKALI KATIKA MAENEO HAYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »