Mwanafunzi afa kwa kutumbukia katika shimo



Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nandanga wa kidato cha kwanza Lukas Msukwa amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la Maji lililochimbwa na watengeneza barabara ya Mpemba hadi Wilayani Ileje, Mkoani Mbeya.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa saba mchana katika Kijiji cha Nandanga, wilaya ya Momba ambapo inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kuteleza na kutumbukia katika shimo hilo lenye urefu wa kina kati ya futi 20 na zaidi ambalo lilikuwa na maji.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa jamii kufunika pamoja na kufukia mashimo yaliyo wazi kwa kuwa ni hatari kwa watoto na hata watu wazima.
Previous
Next Post »