TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.04.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI ETHIOPIA BAADA YA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AITWAE MSUKUMA
PENGO [48] MKAZI WA MTAA WA MWAMBENE ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
JIJINI MBEYA TAREHE 14.04.2014
MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI WAKATI
ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
MAREHEMU ALISHAMBULIWA
KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE, MATOFALI
NA MARUNGU TAREHE 13.04.2014 MAJIRA
YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA
MSIKITI WA SAE, KATA YA ILOMBA, TARAFA
YA IYUNGA. INADAIWA CHANZO CHA TUKIO HILO
NI TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI MOJA AINA YA BAMBUCHA YENYE THAMANI YA TSHS 150,000/= MALI YA IDDY OMARY [37] IMAMU WA MSIKITI WA
SAE, MKAZI WA IGANZO.
AWALI MAREHEMU AKIWA MSIKITINI HAPO ALITOKA NDANI
YA MSIKITI NA KUIBA BAISKELI HIYO WAKATI
IMAMU AKIWA NDANI NA WANANCHI WALIMUONA
KISHA KUMKAMATA NA KUMSHAMBULIA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE
WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI
KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI BADALA YA KUTAKA
UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZA MKATO ZISIZO HALALI KWANI ZINA MADHARA KATIKA
JAMII.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. ABDULSALAM MOHAMED [19] NA 2. ABRUHAMAN HAYALEMASI [28] WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI
ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 14.04.2014 MAJIRA YA SAA
10:50 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA NTENGANO, KATA YA IJOMBE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI KUFUATIA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA WASAMALIA
WEMA KWA JESHI LA POLISI AMBALO
LILIFANIKIWA KUWAKAMATA.TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA
NA RAIA WA KIGENI.
Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon