MTOTO HUYU ATELEKEZWA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI IRINGA



Wakati wakrito duniani leo kusherekea sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo,Pasaka kwa namna mbalimbali, mtoto wa umri zaidi ya miezi miwili ametekelezwa na mama yake katika Hopitali ya Rufa Mkoa ya Iringa jana saa 3 usiku wa kuamkia leo.


Mtoto wa kike wa zaidi ya miezi miwili mwenye uzito wa kilo tano (5kg) ametelekezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoani wa Iringa jana saa 3 usiku wakuamkia leo na mama mmoja na kutokomea kusikojulikana na sasa mtoto amelazwa katika wodi namba 2 kwa uangalizi zaidi. Mtoto huyo anahitaji masaida jamii wa hali na mali ili aweze kusherehekea Pasaka ili afufuke pamoja na Yesu Kristo
 mkombozi wa ulimwengu.


Muuguzi Msaidizi katika wodi ya watoto namba 6, hospitali ya rufa ya mkoa wa Iringa, Olipa Gideon Nyagawa akiwa amembeba mtoto huyo kabla ya kupeleka kwa doktari OPD kwa uchunguzi zaidi baada ya kuona hali ya mtoto inabadilika kwa kuchemka.


Tabibu Mkuu wa hospitali ya rufa mkoani Iringa Dkt. M.M. Ndomba akimchunguza afya mtoto huyo aliyetelekezwa na mama yake hospitalini hapo.


Hawa ni mmoja ya wasamalia wema waliyojitolea kumpatia baadhi ya nguo alizovaa mtoto huyo asubuhi leo baada ya kuguswa na tukio hilo la mama aliyetekekelezwa, walipo kwenda kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali hospitalini leo asubuhi.
Previous
Next Post »