Mcheza mieleka maarufu 'The Ultimate Warrior' afariki baada ya kuanguka ghafla

Mcheza mieleka maarufu aliyetumia jina la The Ultimate Warrior amefariki Jana (April 8) akiwa na umri wa miaka 54, ikiwa ni siku chache baada ya kupewa heshima kwa kuingizwa kwenye WWE Hall of Fame.
WWE imethibitisha kifo chake kupitia website yao na kuandika ujumbe kuonesha jinsi walivyoguswa na msiba huo.
“WWE is shocked and deeply saddened to learn of the passing of one of the most iconic WWE Superstars ever, The Ultimate Warrior. WWE sends its sincere condolences to Warrior's family, friends and fans." Wameandika WWE
Kwa mujibu wa TMZ, mcheza mieleka huyo alipoteza maisha katika eneo la hotel huko Arizona majira ya saa kumi na moja jioni baada ya kuanguka ghafla wakati yeye na mkewe wakitembea kuelekea kwenye gari lao.
Wacheza mieleka wenzake wameandika kupitia twitter jinsi walivyoguswa na msiba wa Warrior.
“RIP WARRIOR. Only love. Ametweet Hulk Hogan.
“Saddened to announce the passing of the Ultimate Warrior. Icon and friend. My sympathy to his wife Dana and his daughters.” Ametweet Triple H.
Warrior ameacha watoto wawili aliozaa na mkewe Dana.
Previous
Next Post »