BREAKING NEWZZ : AJALI MORO BODA BODA AGONGWA NA GARI AVUNJIKA MGUU


Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amegongwa na gari barabara ya zamani ya Dar es salaama jirani na stendi  Katika Manispaa ya Morogoro na kuvunjika mguu wa kushoto. Wakizungumzia Ajali hiyo Mashuhuda wamesema dereva huyo wa boda boda Alikuta gari limesimama baranarani  bila kujua ni kwanini gari la mbele yake limesimama alitanua na kulipita gari hiyo aiana ya Collora na ndipo   kugongana uso kwa uso na gari hilo .
Kijana Huyo ambaye ndiye alikuwa akiendesha bodaboda ndipo alipopata Ajali mbaya iliyompelekea Kuvunjika Mguu wa Kushoto.


 Muendesha Bodaboda Aliyejeruhiwa Vibaya katika Ajali hiyo akipakiwa katika gari kupelekwa Hospitali kwa Matibabu. 

Ajali zinazowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zimeendelea kutawala manispaa ya Morogoro  ambapo Gari Dogo Limegongana na MuendeshaBodaboda .Ajali hiyo imetokea katikati ya Manispaa ya Morogoro ambapo Muendesha Boda boda Alijeruhiwa vibaya.
            Wasamaria wema wakiwa eneo la tukio kutoa msaada mara baada ya ajali hiyo kutokea mapema leo
.







Gari lililogongana uso kwa uso na boda boda huyo
Previous
Next Post »