Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban watu 98, wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama wiki jana katika Ziwa Albert Magharibi mwa Uganda.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, limesema kuwa watu 41 wameokolewa na wengine wengi bado hawajapatikana.
Boti hiyo ilikuwa imewabeba wakimbizi wa DRC waliokuwa wanarejea makwao kutoka katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa umewarejesha manusura nchini Uganda ambako wanapokea msaada
CHANZO: BBC
EmoticonEmoticon