Urusi kufanya mazungumzo na Iran leo kuhusu ujenzi wa vinu vingine vya nuclear nchini Iran


Wakati ambapo Marekani na washirika wake waliiwekea Iran vikwazo vya kibiashara kwa madai ya kutengeneza nishati ya nuclear kinyume cha sheria za kimataifa, imeripotiwa kuwa leo (March 11) Urusi itafanya mazungumzo na Iran kuhusu kuisaidia kujenga vinu vingine vya nuclear nchini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa radio ya Urusi, Voice of Russia, Mkurugenzi msaidizi wa mambo ya nje wa Urusi katika masuala ya nishati za Atomi, Nikolai Spassky ataingia Iran leo na kufanya mazungumzo na maafisa wa Iran kuhusu ujenzi wa vinu vipya vya nuclear katika eneo la Bushehr.
“Mpango wentu ni kujenga vinu vinne katika eneo la Bushehr, na tunatakiwa kuangalia jinsi ambavyo mazungumzo yataendelea.” Amesema msemaji wa shirika la nishati za atomi, Behrouz Kamalvand.
Hata hivyo maafisa wa Urusi bado hawajaeleza wazi kuhusu kuwepo kwa mazungumzo hayo leo ama la, huku wakisisitiza kuwa hawavunja vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Mwezi uliopita, balozi wa Iran nchini Urusi, Mehdi Sanaei alisema kuwa nchi hizo ambazo zishirikiana kwa karibu katika masuala ya biashara zimekubalina kuhusu Iran kuipa mafuta mengi Urusi kwa malipo ya huduma nzuri na bidhaa.
Previous
Next Post »