Taarifa zilizotangazwa na Waziri mkuu wa Malaysia, imefahamika ndege iliyopotea ilianguka baharini na wote wamefariki.


Screen Shot 2014-03-24 at 7.02.59 PM
Baada ya uchunguzi wa muda mrefu kuitafuta ndege ambayo ilidhaniwa kuwa imepotea au kupatwa na matatizo mengine baada ya kushindwa kufika sehemu iliyotakiwa kwa wakati, taarifa za uchunguzi mpya zilizotangazwa na waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak,  imefahamika ndege hii Malaysia Airlines ilidondoka kusini mwa bahari ya hindi.
Kutokana na uchunguzi wa ziada uliofanyika na data zilizopatikana kutoka kwa shirika la Uingereza linalojihusisha na uchunguzi wa ajali, sasa  hivi hakuna matumaini ya kupona kwa abiria yeyote kwenye ndege hiyo.
mal
Ndugu wa abiria ambao walikuwa Beijing kusubiri ndege hiyo wanasema wametumiwa meseji na shirika hilo ikisema ndugu zao wote wamefariki kwenye hiyo ajali.
Waziri mkuu huyo Najib Razak hakuelezea zaidi kwa undani juu ya ajali hiyo lakini kingine ambacho alikisema ni kwamba ndege hii ilianguka katikati ya bahari na hakukua na ardhi yoyote ya karibu ambayo ingeweza kutua.

http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/Screen-Shot-2014-03-17-at-11.49.52-PM.png
  
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak. 


SHIRIKA la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura. Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.

Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.

Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko.

Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.

Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.

Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.

Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita. Ndege na meli za nchi mbali mbali zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.

BBC
Previous
Next Post »