Sidiria zinazotoa umeme kuzuia ubakaji
Kundi la wanafunzi nchini India limefanikiwa kutengeneza sidiria za umeme ili kuwafanya wanawake waweze kujilinda wakati wa matukio ya ubakaji kwa kuwapiga shoti wabakaji.
Sidiria hizo za umeme zina uwezo wa kumpiga shoti mtu kwa umeme wa kiasi cha 3,800kv.
Sidiria hizo mbali ya kutoa shoti ya umeme unaotengenezwa na kifaa kwenye sidiria kinachotumia betri pia zina uwezo wa kutuma ujumbe wa meseji kwenda kwa mtu anayetakiwa kujulishwa juu ya tukio hilo na pia kutuma maelekezo ya sehemu ya eneo la tukio.
Wanafunzi hao wa India katika chuo kikuu cha mji wa Chennai walitengeneza sidiria hizo baada ya kubakwa kwa mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 23 katika mji wa Delhi. Mwanafunzi huyo alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kubakwa na kundi la wanaume wengi kufuatia tukio hilo lililotokea mwezi disemba mwaka jana.
Wanafunzi hao wa India waliamua kufanya utafiti wa kutengeneza sidiria kama hizo ili ziweze kuzuia matukio mengine ya ubakaji yasitokee.
Sidiria hiyo imewekewa kitu cha kutathmini ukubwa wa presha ya kukandamizwa ili kuifanya sidiria hiyo iweze kuruhusu kutolewa kwa shoti ya umeme.
Presha ya mgandamizo kwenye kifua kutokana na kukumbatiana haitaifanya sidiria hiyo iruhusu kutolewa kwa shoti ya umeme.
Ili kumlinda mvaaji, sidiria hiyo imetengenezewa material maalumu yatakayozuia umeme kumrudia mvaaji.
EmoticonEmoticon