HATIMAYE mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, amechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Bunge hilo huku akijigamba kuwa hatatawaliwa na hisia za chama au binafsi katika kukiongoza chombo hicho.
Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu unatarajiwa kufanyika leo jioni huku Sitta akipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kutosimamisha wagombea.
Katika kinyang’anyiro hicho, Sitta, atapambana na kada mwenzake kutoka CCM, Terezya Huvisa, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), pamoja na Hashim Rungwe, kutoka Chama cha Umma (Chauma).
EmoticonEmoticon