SABABU KWA NINI WAPENZI WAKIISHI MUDA MREFU PAMOJA HUFANANA!



Umewahi kujiuliza au kujipatia picha wewe ukizeeka utaonekanaje? Mtazame baba yako au mama yako, alivyo ndivyo wewe utakavyokuwa.

Anyways...

Kuna 'concept' fulani iliyojengeka miongoni mwa jamii kwamba watu wawili, mfano mume na mke wakiishi muda mrefu pamoja huishia kufanana sura zao. Je, unaamini hiyo 'concept'? 


Baada ya kuona ni jambo ambalo linahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi, wataalamu wa 'weird researches' Bwana Robert Zajonc na wenzake waliamua kufanya utafiti wa kina ili kugundua ukweli wa 'concept' hiyo.

Hivi ndivyo walivyofanya:

Walichukua washiriki wapatao 110 na kuwaonesha picha za wanandoa tofauti tofauti wakiwa katika miaka ya mwanzo mwanzo ya ndoa zao. Halafu baadae zikachukuliwa picha za wanandoa hao hao miaka 25 baada ya ndoa zao. Picha hizo zilikatwa na kila moja kuchanganywa na nyingine bila kujali nani amemuoa au kaolewa na nani. 

Majibu yalionesha kwamba asilimia 70 ya waliooneshwa picha hizo walifanikiwa kufananisha angalau asilimia 80 ya wanandoa hao, na hivyo kufikia 'research' hiyo kukubali kuwa ni kweli watu wakiishi pamoja muda mrefu hufanana.

Lakini swali walilojiuliza ni 'why'? Kwa nini? Wataalamu hao walikuja na majibu yafuatayo:

1. Diet (Mlo): Kama mna-share chakula cha aina inayofanana kwa muda mrefu, kuna uwezekano mkubwa wa chakula hicho kuwapatia aina sawa za madini ambazo zinafanya kazi ya ku-develop body features, including sura yako. e.g if both partners eat a high fat diet, both their faces will tend to look chubby. 

2. Environment (Mazingira): Kama mnaishi kwenye eneo moja kwa muda mrefu, hali ya hewa, mwanga wa jua, baadhi ya 'chemicals' au gesi zinazozunguka maeneo hayo zinaweza kuwa na matokeo yanayofanana katika mwili wa binadamu, sura ikiwa ni moja ya maeneo ambayo huguswa zaidi.

3. Predisposition: Hii ni hali ya ukweli kwamba watu wengi hupenda kuchagua 'partners' ambao wanaendana aidha kimaumbile au kimuonekano. Kama ukichagua partner mwenye sura ya huzuni huzuni hivi kama wewe, kuna uwezekano mkubwa baadae ukawa na sura iliyo 'depressed' kama yake.

4. Empathy (Hisia za ndani kabisa kumuelekea mwenzako): Kutokana na kutumia muda mwingi kuoneshana mapenzi kwa sura hasa wakati watu 'wanapetipetiana' hivi wakati ambao hadi sura huwa zinabadilika na kuwa zilizojaa mapenzi mazito, hiyo ni mojawapo ya sababu inayofanya watu wawili walioishi muda mrefu kufanana.


Na utafiti huu kwa kutumia pointi hii namba 4, ilikuja na matokeo mengine makubwa zaidi ambayo yalithibitisha kuwa wanandoa waliokuja kufanana nyuso zao baada ya kuishi muda mrefu, ndio wanandoa waliokuwa na ndoa yenye furaha zaidi, kutokana na kile kilichoelezwa katika pointi namba 4.
Previous
Next Post »