PISTORIUS:SEHEMU YA USHAHIDI KUBANWA

AP_oscar_pistorius_reeva_steenkamp_jt_140302_16x9_992_898e1.jpgMashahidi wa upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji dhidi ya Oscar Pistorius wanaendelea kutoa ushahidi zadi dhidi ya mwanariadha huyo katika wiki ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Upande wa mashitaka unanuia kuthibitisha kuwa bwana Pistorius alimpiga risasi maksudi aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka jana wakati wawili hao walipokuwa wanagombana.
Pistorius amekanusha madai hayo akisema kua alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yao.
Mtaalamu wa uchunguzi wa mauaji Gert Saayman anatarajiwa kutoa ushahidi kuhusu majeruhi aliyoyapata Reeva kabla ya kifo chake ingawa ameitaka mahakama kutoonyesha picha hizo kutokana na athari zake na pia kumsitiri mwathiriwa ambaye ni marehemu Reeva.
Wakati huohuo jaji anayesikiliza kesi hiyo amepiga marufuku kupeperusha kesi dhidi ya Oscar moja kwa moja kutoka mahakamani wakati ambapo picha za mauaji ya Reeva zitakaponyeshwa.
Pistorius alitapika mahakamani aliposikia ushahidi kuhusu mauaji ya Reeva na kuona picha hizo.
Bwana Saayman alimshawishi jaji kutoruhusu kuonyeshwa kwa picha hizo akisema kuwa zinaonyesha majeruhi mabaya aliyoyapata Reeva na kwamba ni lazima mahakama iweze kumsitiri marehemu.
Jaji huyo pia alipiga marufuku mjadala wowote kuhusu picha hizo kwenye Twitter.
Previous
Next Post »