NYOTA WA MAN UNITED KUINUNUA SALFORD CITY.


Nyota wa Man United kuinunua Salford City.










Nyota wa zamani wa Manchester United,Neville,Phil 


Neville,Ryan Giggs,Paul Scholes na Nicky Butt wamekubaliana kufanya mchakato wa dili la kuinunua klabu ya Salford City.
Suala hilo limekuja na limeleta maswali kwa Chama cha soka nchini Unigereza,FA pamoja na bodi inayoendesha ligi.
Mustakabadhi wa dili hilo unataraji kukamilika baadae msimu huu juu ya kuinunua klabu hiyo iliyopo kaskazini ikishiriki ligi daraja la chini kabisa.
Uthibitisho wa dili ambao umekuwa tetesi kwa wiki kadhaa umekuja siku ambayo Man United walipokanusha taarifa kuwa kizazi hicho cha miaka ya 1992 kilitaka kuchukua nafasi ya kuinoa klabu hiyo ya Old Trafford.
Kundi la nyota hao limekuwa imara na wanataka kurudisha kitu flani kikubwa kwenye umoja wa Salford na maeneo yote yanayoizunguka.
Huku Giggs akiwa bado ni mchezaji wa Man United,Phil Neville akisaidiana na David Moyes kwenye benchi la ufundi na kaka yake,Gary akifanya kazi kwenye kituo Sky Sports lakini haijajulikana zaidi wamejiwekea malengo mbele mara watakapofanikiwa kuichukua timu hiyo.
Pia inasemekana hawatafanya mabadiliko yeyote ya uongozi wa Salford City ambayo uwanja wake wa nyumbani upo Moor Lane mjini Kersal.
Gary Neville alisema kuwa,”Nilikuwa na kipindi kizuri sana kwa Manchester United ndani Salford nikiwa na umri wa miaka 11 na siwezi kusahau jinsi ilivyokuwa na umuhimu kwangu.”
Scholes akasema,”Tunafahamu itakuwa na ugumu sana lakini tutakuwa imara kwa hili kuanzia mwanzo na kuwa na mipango madhubuti zaidi na kuitekeleza.”
Butt naye aliongeza kuwa,”Moor Lane pamekuwa mahala salama kwa miaka 320 iliyopita ikiwa ni eneo la Manchester hii ingepaswa kulindwa na kuheshimiwa hivyo imekuwa kitu kizuri kwa manufaa ya baadae.”
Phil Neville naye akasema,”Ni muhimu kulinda kazi ngumu iliyofanywa ndani ya ligi dogo zaidi na inaenda kuwa imara kwa kutumia uzoefu wetu na kusaidia wachezaji chipukizi.”
Giggs alimaliza kwa kusema,”Kila mtu anajua jinsi gani Salford ilivyokuwa muhimu kwangu hivyo hiki ni kitu kinachodumu na sahihi kabisa na wote tunaamini hilo.”
Mwenyekiti wa Salford City,Karen Baird ambaye alizungumzia dili hilo na kusema kuwa,”Ni kipindi kizuri sana kwa Salford City FC na naamini kuna mambo makubwa mazuri na mafanikio zaidi yanakuja kwa klabu,hakuna shaka lolote dili hili litatoa matokeo ya kuleta mwanga kwenye ligi ambayo haijulikani kabisa.”
Previous
Next Post »