Mwanamke huyu ashitakiwa kwa kumuua mwanae wa miaka 4 baada ya kuhisi ni 'shoga'



Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Jessica Dutro, anakabiriwa na kesi ya mauaji huko Washington Marekani baada ya kutuhumiwa kuwa alimpiga mwanae wa miaka 4 hadi kumuua baada ya kuhisi kuwa atakuwa ‘shoga’. 
Waendesha mashitaka walidai kuwa August 14, 2012 mama huyo aliwapiga vibaya watoto wake watatu, lakini kipigo kilikuwa kikali zaidi kwa mwanae aitwae Zachary Dutro- Boggess ambaye alimuudhi zaidi baada kuona kuwa anatabia za kishoga mapema akiwa mtoto.Baada ya kipigo kikali mtoto huyo alipelekwa hospitalini siku hiyo na kitengo cha dharura na kuwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua, hata hivyo baada ya siku mbili alipoteza maisha Ushahidi uliofikishwa mahakamani mwanzoni mwa mwezi huu na muendesha mashitaka, Megan Johnson unaonesha kuwa ujumbe wa Facebook aliotuma mwanamke huyo kwenda kwa mpenzi wake aitwae Brian Canady ndio uliobeba sababu ya chanzo cha kichapo kikali alichopewa mtoto huyo. Alimueleza kuwa mtoto wake anaelekea kuwa shoga. “Anatembea na kuongea kama vile (shoga). Ugh.” Ilisomeka sehemu ya ujumbe huo uliokuwa ukimueleza mpenzi wake huyo kuwa anampiga mwanae muda huo. Kutokana na majibishano ya kwenye Facebook, mpenzi wake huyo pia alifunguliwa mashitaka na mahakama ikamkuta na hatia mwanzoni mwa mwezi huu kwa mchango wake kufuatia kifo cha mtoto huyo, kwa kuwa ujumbe mmoja ulionesha kuwa mwanamke huyo alimpa jukumu la kumfanyia kazi mtoto huyo.
Previous
Next Post »