JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.cmbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 20.03.2014.
·
MTOTO WA MIAKA 07 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA
NA BABA YAKE MZAZI.
·
MTU MMOJA AUAWA BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA
WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA
NA GARI KATIKA AJALI YA BARABARANI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
RAIA WA KIGENI WATANO KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MTOTO AITWAYE IREENE
MARCO MBEMBELA (07) MWANAFUNZI CHEKECHEA SHULE YA MSINGI MIGOMBANI NA MKAZI
WA SOGEA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA
AFYA TUNDUMA.
MAREHEMU ALIPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI
ZA MWILI WAKE HADI KUPOTEZA FAHAMU NA
BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA MARCO MBEMBELA (30) MKAZI WA
SOGEA – TUNDUMA.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.03.2014 ALFAJIRI HUKO SOGEA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA
MOMBA KWA TUHUMA KUWA ANATABIA YA
KUZURURA OVYO KATIKA NYUMBA ZA WATU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUTUMIA BUSARA KATIKA KUWAELEKEZA NA KUWAONYA
WATOTO WAO BADALA YA KUWAPIGA KWANI NI HATARI KWA AFYA NA MAISHA YAO.
PIA HUKO
WILAYA YA KYELA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MATESO LAMSI (25) MKAZI WA KIJIJI CHA NDOBO ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA MARUNGU.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 18.03.2014 SAA 20:00 USIKU
KATIKA KIJIJI CHA NDOBO, KATA YA NDOBO, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUKAMATWA AKIIBA
KAKAO KWENYE SHAMBA LA JAPHET MWAKALINGA.
MAREHEMU ALIKUWA MHALIFU MZOEFU NA AMETOKA GEREZANI
HIVI KARIBUNI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO WAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
AIDHA KATIKA
TUKIO JINGINE:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GODFREY KAYANGE (22) FUNDI MAGARI, MKAZI WA MAKAMBAKO ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI
WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
WILAYA MBARALI BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.859 AGL/T.650 AKB AINA YA SCANIA
TRUCK LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA BENJAMIN
MANDELE (38) MKAZI WA MAFINGA.
AJALI HIYO ILITOKEA TAREHE 19.03.2014 SAA 16:00
JIONI KATIKA KIJIJI CHA MKOMBE, KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DEREVA KUTOKUMUONA
MAREHEMU WAKATI AKIDANDIA GARI HILO NA KUMGONGA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI
LIPO KITUO CHA POLISI RUJEWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA ENEO LA KASUMULU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WA
PAKISTAN WATANO AMBAO NI 1. MOHAMED RASHID (35), 2. SADAM HUSSEIN (19), 3.
NAWICED IGBILI (23), 4. GULU LAZA (31) NA 5. MUZZAFAR HAMED (24) WOTE WAKAZI WA
NCHINI PAKISTAN WAKIWA WAMEINGIA NCHINI
BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO HARAMU WALIKAMTWA TAREHE 18.03.2014 SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA ENEO LA KASUMULU, KATA YA NGANA, TARAFA YA
UNYAKYUSA WILAYA YA KYELA. WATUHUMIWA
WAMEKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI
ZAIDI UFANYWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon