MHE.ANGELLAH KAIRUKI PAMOJA NA MWANZILISHI WA BONGO5 WATEULIWA KUWA VIONGOZI VIJANA DUNIANI ‘YOUNG GLOBAL LEADERS 2014′.


Image
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angellah Kairuki  (kushoto) pamoja na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji (CEO) wa Bongo5 Media Group na Jefag Logistics Tanzania Ltd, Luca Neghesti (chini) wameteuliwa kuwa miongoni mwa viongozi vijana duniani, ‘Young Global Leaders 2014’.
Watanzania hao wawili wameingia kwenye jopo hilo ambalo mwaka huulinaundwa na vijana 214 kutoka nchi 66 duniani kutoka serikalini na makampuni binafsi.
Mwaka huu Afrika ina wawakilishi 19 peke yake.Idadi hiyo imepatikana kufuatia maombi kutoka kwa watu zaidi ya 5,000 waliopendekezwa kutoka duniani kote na hatimaye kuchaguliwa baada ya mchujo mkali na kamati maalumu iliyo chini ya uenyekiti wa Malkia wa Jordan, Rania Al Abdullah. 
 Young global leaders ni vijana chini ya miaka 40 wanaosifika kwa michango yao katika jamii na pia ni viongozi wadogo kwenye maeneo yao ya kazi na wameweza kufikia uongozi ndani ya muda mfupi na pia kutokana na Ustawi wao wa kijasiriamali. 
Neghesti amepata nafasi hiyo kutokana na mafanikio ya kiujasiriamali kupitia Bongo5 Media Group, KINU na JEFAG logistics na DICD (Dar es salaam Inland Container Depot). 
Watanzania wengine waliowahi kuchaguliwa kwenye jopo hilo ni pamoja na January Makamba, Mohammed Dewji, Elsie Kanza, Lawrence Masha na Susan Mashibe.
Previous
Next Post »