JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.cmbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.03.2014.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO
KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
·
MAHABUSU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJARIBU
KUJINYONGA KWA KUTUMIA SHATI LAKE.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA
WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
·
GARI AINA YA NOAH [IT] YAIBWA HUKO WILAYANI
MOMBA – TUNDUMA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
MFANYABIASHARA MMOJA AKIWA ANAMILIKIA SILAHA KINYUME CHA SHERIA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA KYELA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU
KIZITO KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MCHIMBI
ALADI (34) MKAZI WA KIJIJI CHA MNAZI ALIKUTWA AMEUAWA
KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE
KUTUPWA KATIKA MTO RUAHA. TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KITONGOJI CHA
IGUNULA, KIJIJI CHA MNAZI, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI. CHANZO CHA
MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA UCHAWI. MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA INNOCENT NKWANDA (24) MKAZI WA WILAYA YA MBOZI AMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA
WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ILI
WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MAHABUSU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUJARIBU KUJINYONGA KWA KUTUMIA SHATI LAKE.
MAHABUSU MMOJA AITWAYE NASSON
PAULO [70] MKAZI WA RUIWA WILAYANI MBARALI MKOANI MBEYA ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA
KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUJINYONGA
AKIWA MAHABUSU KATIKA KITUO CHA POLISI
KATI MBEYA MNAMO TAREHE 17/03/2014
MAJIRA YA SAA 04:50 ALFAJIRI KUTOKANA
NA TUHUMA ZA MAUAJI.
MAREHEMU HUYO
ALIKAMATWA KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAUAJI INAYODAIWA KUYAFANYA TAREHE 12.02.2014 KWA KUMUUA KWA KUMPIGA
NYUNDO KICHWANI DONALD JOSEPH@ YUSUPH ALIYEDAIWA KUMUIBIA NG’OMBE WAKE NA KISHA
KUFICHA MABAKI YA MWILI WAKE KUSIKOJULIKANA.
MAREHEMU NASSON PAULO ALIKAMATWA BAADA YA KUPATIKANA KWA USHAHIDI TOKA
KWA WATU WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO LA MAUAJI NA ALIPOHOJIWA ALIAHIDI KWA
WAPELELEZI KUWA SIKU INAYOFUATA YAANI TAREHE 17.03.2014 ATAKWENDA KUONYESHA ENEO ALIPOPELEKA MWILI HUO. MTUHUMIWA
ALIRUDISHWA MAHABUSU.
MNAMO MAJIRA YA SAA 04.50 ALFAJIRI WAKATI MTUHUMIWA
AKIWA MAHABUSU CHUMBA CHA PEKEE YAKE KUTOKANA
NA UMRI WAKE NDIPO ALIFANYA JARIBIO LA KUJINYONGA KWA KTUMIA SHATI YAKE. HATA
HIVYO ASKARI WA ZAMU WALIFIKA NA KUMKUTA
CHINI AKIPUMUA KWA SHIDA HALI ILIYOWAFANYA WAMKIMBIZE HOSPITALI YA RUFAA KWA MATIBABU
YA HARAKA LAKINI HAKUWEZA KUCHUKUA MUDA MREFU NA HATIMAYE ALIFARIKI DUNIA.
MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI
WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL
MWASUNDA (39) MFANYABIASHARA,
MKAZI WA MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA
NA KUPINDUKA. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 17.03.2014 MAJIRA YA SAA
15:00 ALASIRI KATIKA KIJIJI CHA ISALALO, KATA NA TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI BARABARA YA MLOWO/MSANGANO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.634 CTN AINA YA MITSUBISHI FUSO TIPPER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE KUACHA NJIA NA KUPINDUKA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO
HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,
VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
GARI AINA YA NOAH [IT] YAIBWA HUKO
WILAYANI MOMBA – TUNDUMA.
GARI
LENYE NAMBA IT 1163 AINA YA TOYOTA NOAH RANGI NYEUPE ILIYOKUWA
IKISAFIRISHWA NA KAMPUNI YA TRIPPLE D KWENDA NCHINI ZAMBIA AMEIBWA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 HUKO
KATIKA MTAA WA SOGEA - TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA.
GARI HIYO ILIIBWA WAKATI IKIWA IMEEGESHWA KATIKA BAR IITWAYO MSASANI BAADA YA WATU HAO KUMVAMIA MTU ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA BENSON SIMUMBA (56) MLINZI KAMPUNI YA PANIC SYSTEM
GROUP NA KISHA KUMFUNGA KAMBA NA KUIBA GARI HILO. AIDHA WATU HAO WALIMJERUHI
KWA KUMKATA MAPANGA KWENYE PAJI LA USO NA KISOGONI HAMIS MLONDWE YANDA (31)
MKUSANYA USHURU WA ENEO HILO, MKAZI WA MTAA WA MWAKA -TUNDUMA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MFANYABIASHARA MMOJA AKIWA ANAMILIKIA SILAHA KINYUME CHA SHERIA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MFANYABIASHARA MMOJA AITWAYE MAULID JULIUS MWANGILA (43) MKAZI WA MTAA WA
MWAKA-UWANJANI TUNDUMA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA MOJA AINA YA
BASTOLA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI INAYOTUMIA RISASI ZA S/GUN. MTUHUMIWA
ALIKAMATWA TAREHE 17.03.2014 MAJIRA
YA SAA 02:00 USIKU KATIKA MTAA WA
MWAKA- UWANJANI – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA KATIKA
MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. UPELELEZI UNAENDELEA NA UTAKAPO KAMILIKA
NA KUTHIBITIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUMILIKI SILAHA, VINGINEVYO
WASALIMISHE WENYEWE SILAHA HIZO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KYELA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU
NA SERIKALI.
MTU
MMOJA AITWAYE BARAKA ADAM (27) MKAZI WA KYELA KATI ANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI AINA YA BWANA GIN KATONI 27
KUTOKA NCHINI MALAWI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:30
ALASIRI KATIKA MTAA WA KYELA MJINI, KATA YA KYELA –KATI, TARAFA YA
UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA KATIKA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA
KUMKAMATA NA KAMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MTU YEYOTE ATAKAYE BAINIKA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HIYO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon