HIZI SABABU KWANINI MOYES HAFAI KUENDELEA KUIFUNDISHA MAN UNITED


Manchester United lazima imtimue David Moyes mwishoni mwa msimu huu. David Moyes hana uwezo wa kuiongoza Manchester United kuendeleza mazuri ya aliyemrithi na kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio, jambo ambalo ndilo linalotegemewa katika klabu ya ukubwa wa United. 

Badala ya kuendelea uongozi mbovu wa Moyes, klabu inabidi ubora na uimara wa timu kupitia kocha na benchi la ufundi ambalo huko nyuma tayari wameshaongoza timu kwa mafanikio. United ina ufuasi mkuwa wa mamilioni ya mashabiki duniani kote na kutokana na hili United inastahili kupata uongozi bora zaidi kuliko huu wa Moyes. 

Sababu kwanini Moyes aondoke Manchester United: 

Kukosa uzoefu wa kushinda - Moyes hajawahi kushinda kombe katika career yake ya ukocha - ukiondoa kombe la nguo la hisani, ambalo alikuta timu yake imeshafikishwa kwenye mchezo huo tena dhidi ya timu ya ligi ya daraja ya kwanza ya Wigan. 

Ukosefu wa uwezo wa kufundisha wachezaji wakubwa - Ukweli wa kwamba hajawahi kuwa na bahati ya kuwa na kikosi chenye wachezaji wakubwa unamaanisha kwamba hajui namna nzuri ya kudili na aina ya wachezaji wa aina hiyo, kuwafurahisha na kuwapa motisha au kujua namna ya kupata kiwango kilicho bora kutoka kwao. Ni vigumu kutegemea wachezaji walioshinda kila kitu na matajiri kumheshimu kocha ambaye hajawahi kushinda kitu chochote. 

  Ukosefu wa uzoefu wa kudili na mategemeo makubwa - Baada ya kuwa Everton kwa miaka 11, mahala ambapo alikuwa akifaulu kumaliza ligi katikati mwa msimamo akiwa na bajeti ndogo ya usajili, Moyes hana uzoefu wa kudili na presha ya mategemeo makubwa ambayo huja pamoja na kazi yake ndani ya United - na hilo tayari limeshaonekana.  

Mbinu zilizopitwa na wakati - Ukosefu wake wa mbinu bora mwanzoni na kati kati ya mchezo zimeigharimu sana timu msimu huu. Baada ya mechi ya Fulham Rene Maulesteen alisema ilikuwa kazi rahisi sana kucheza na United yenye mbinu zilezile zilikosa mabadiliko, pia beki wa kati wa Fulham Dan Burn alizidharau mbinu za Moyes kwamba zilikuwa rahisi sana kuzuia. Akiichezesha timu kwa mfumo wa kizamani 4-4-2 - timu haionyeshi kuwa na maendeleo bora katika kipindi cha miezi tisa ya utawala wake, lakini pamoja na haya yote bado haonekani kulitambua tatizo hili la mfumo na kulitafutia ufumbuzi. 

Wasaidizi wabovu - Makocha wasaidizi wa United chini ya Sir Alex walikuwa Meulensteen, Mike Phelan na Eric Steele. Wote kwa pamoja walikuwa na uzoefu wa ukocha wa level ya juu kwa miaka 25 na walikuwa walikuwa wanajua namna ya kuwaandaa vijana kushinda mechi na kushinda makombe. 

Uamuzi wa Moyes kuwaondoa hawa wasaidizi umezidi kuwa mbovu baada ya kuwaleta wabadala wao: Phil Neville (hakuwa mchezaji wa daraja la juu, hana uzoefu mzuri wa ukocha zaidi ya kuhusika na timu ya  England U21, ambayo ilikuwa ikifanya vibaya), Steve Round (alikuwa mmoja ya makocha walioishusha timu mpaka daraja la kwanza kutoka EPL, hana uzoefu wa kufundisha timu kubwa), Ryan Giggs (mchezaji wa daraja la juu - lakini ni kocha ambaye hana uzoefu), na Moyes mwenyewe (mbinu zake hasi - anaendekeza zaidi mazoezi magumu badala ya mazoezi ya kiufundi). Je watu hawa wana uwezo na wanafaa kuliongoza benchi la ufundi na kupata kilicho bora kutoka kwa wachezaji wa hadhi ya juu, na kwa mtazamo wa sasa inaonekana jibu ni hapana, wameishindwa kazi hiyo. 

Namna mbovu ya kudili na vyombo vya habari - Namna Moyes anavyodili na vyombo vya habari tangu sio sawa kabisa tangu alivyofika Old Trafford. Hana approach nzuri - Amekuwa akisisitiza kwenye jibu moja kwamba timu ina "bahati mbaya" na kurudia rudia msemo wake wa "Nadhani tumecheza vizuri" (Timu iwe imefungwa, imeshinda, au suluhu) - hii kauli inaonyesha ambition. 

Manchester United inabidi isiwe na mtazamo wa kukubali suluhu au vipigo kwa namna Moyes anavyochukulia. Inabidi tutegemee ujuzu, mbinu, na nguvu katika kutafuta ushindi kuliko kutegemea bahati kama Moyes anavyosema. 

Usajili - Jaribio la kusajili wachezaji wakubwa dirisha kubwa la usajili lilopita lilionyesha kufeli. Baada ya hapo akamleta Marouane Fellaini (kwa £27.5m, £4m zaidi ya fedha ambayo angeweza kumsajili kabla) kuja kucheza kama kiungo mkabaji. 

Moyes alifanya kazi na Fellaini kwa miaka kadhaa Everton na kwa maana hiyo alikuwa akijua kabisa uwezo wa kucheza kwenye hiyo nafasi na aliamini angeweza kucheza. 

Hata hivyo, ameonekana hayupo ccomfortable kuicheza nafasi hiyo kwa kuangalia kiwango chake mpaka sasa - hivyo haukuwa usajili mzuri kwa United.  Usajili Juan Mata umekuwa wa kuvutia, lakini ukweli unabaki kwamba Wayne Rooney anacheza kama namba 10, nafasi ambayo Mata huicheza kwa ubora, hivyo matokeo yake Mhispania huyo huchezeshwa pembeni.

 Mata anakosa mbio na nguvu ya kucheza kama winga asilia, hivyo Moyes anavyoendelea na mfumo wa 4-4-2 sioni mabadiliko chanya ya kupata kilicho bora kutoka Juan Mata. 

Akiwa tayari kashatumia kiasi cha £65.5m huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyte yanayoonekana katika kiwango cha timu, United haipaswi kumuamini Moyes na fedha zao katika dirisha la usajili lijalo pia kutegemea yeye na wasaidizi wake kupata kilicho bora kutoka wachezaji waliopo na watakaosajiliwa.  


Moyes amekuwa akivunja rekodi nzuri kwa matokeo mabaya kila kukicha. Ile hali ya timu kuiogopa Man United iliyojengwa kwa miaka mingi iliyopita imeondoka ndani ya miezi michache. Akiwa na rekodi mbovu kuliko zote dhidi ya timu za Top 6 kama kocha wa Everton, ilikuwa wazi kwamba Moyes hana uwezo wa kuiongoza United.

 Hali inaonekana itaendelea kuwa hivyo wakati wote Moyes atakapoendelea kuwa kocha - uongozi wake ndani ya United dhidi ya timu za Top 6 msimu huu ameambulia pointi sita tu - akiambulia sare 3 na ushindi mmoja tu. Mechi dhidi ya timu kubwa kwenye ligi ni muhimu sana - kwa pointi pia kisaikolojia. 

Huku United wakishindwa kuzifunga timu hizi, inaonekana wazi ni vigumu kwa United kupata mafanikio chini ya Moyes. 
SOURCE -shaffih dauda
Previous
Next Post »