TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.03.2014.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA
PIKIPIKI MOJA MALI YA
WIZI NA VIFAA MBALIMBALI VYA KOMPYUTA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 14.03.2014
MAJIRA YA SAA 04:00 USIKU HUKO KATIKA
ENEO LA VWAWA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI LAKAMATA PIKIPIKI
MOJA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.575 CET AINA YA
T-BETTER, CPU KUMI [10] ZA KOMPYUTA PAMOJA NA KEY BOARD MOJA MALI ZA WIZI.
KATI YA MALI HIZO CPU ZIMETAMBULIWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA KUONA
ASKARI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
AIDHA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA
TAREHE 14.03.2014 MAJIRA YA SAA 06:30 ALFAJIRI KATIKA ENEO LA
IYELA-AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA
WA MBEYA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANSIS JOHN (21) MKAZI
WA IYELA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE 04 SAWA NA UZITO WA GRAM 20. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA
BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYIKA IKIWA NI PAMOJA NA KUMFIKSHA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ILI MTUHUMIWA WA TUKIO LA WIZI AWEZE
KUKAMATWA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMIII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon