HABARI TOFAUTI ZINAZO CHANGANYA KUHUSU UKWELI WA KUPOTEA KWA NDEGE YA MALAYSIA

Maswali yamebaki bila majibu kwa muda mrefu sasa lakini cha kushangaza ni jinsi taarifa zinavyobadilika kila siku kuhusiana na nini kimetokea kwa ndege hii.

Jambo la kwanza ilisemekana ndege imeangushwa na magaidi na tukaoneshwa kuna abiria wawili wenye asili ya taifa la Iran ambao walipanda ile ndege na pasi bandia. Bahati mbaya picha zilizotolewa zilionesha kitu cha ajabu sana, abiria wale wawili picha zao ambazo zilipigwa dakika chache kabla ya kupanda ndege zilionesha kufanana moja kwa moja tokea kwenye kiwiliwili hadi chini. Wazo la Ugaidi likaanza kufa.

Jambo la pili, tumepewa sayansi kuwa ndege ilipotea ghafla kwenye Radar za Malaysia ikimaanisha hapo ndipo ndege ilipoanguka. Kwa bahati nzuri wote tunajua kila nchi ina jeshi na moja ya jukumu la jeshi ni kulinda mipaka ya nchi, ardhini, majini na angani. Jeshi la Malaysia alikuwa likizo, taarifa ni kwamba baada ya ndege kupotea kwenye radar za kiraia za Malaysia iliendelea kuonenakana kwenye radar za jeshi kwa takribani saa nzima ikionekana kubadili uelekeo na kuelekea magharibi hadi ilipokaribia milango (Straits) ya Malacca ndipo ilipopotea kwenye radar ya jeshi. Wakati ndege inapotea kwenye radar za kiraia ilikuwa inaruka futi 36,000 lakini kwa mujibu wa radar ya jeshi, ikiwa Malacca ndege ilikuwa umbali wa futi 29,500 kutoka usawa wa bahari. Kuna baadhi ya wataalam wameeleza kuwa kutoonekana kwenye radar ya kiraia kulisababishwa na kuzimwa kwa kifaa kinachofahamika kama Transponder yaani kitambulisho cha ndege kwenye radar. Kwa wanaofahamu vizuri masuala ya ndege watanielewa vyema, hiki kifaaa ni kitambuzi tuu na hakiusiani na kuonekana ama kutoonekana kwenye radar na ndio maaana kinapatikana kwenye baadhi tu ya ndege. Kuna maelfu ya ndege zinaruka bila kuwa na hiki kifaa. Kwa sheria za anga ndege kubwa za abiria ni lazima zifungwe transponder. Tukirejea kwenye radar, hii kazi yake ni kutambua chochote kinachoruka kwenye anga la eneo husika iwe ni ndege, puto au zile drones. Kutokana na hili, sababu iliyotolewa kuhusu transponder ilipotoshwa mno tena na vyombo vingi vya habari vya kimataifa na hata wachambuzi mbalimbali kwenye hili tukio. Ndio maana radar za jeshi ziliweza kuendelea kuiona iyo ndege pamoja na madai ya transponder kuwa off.

Jambo la tatu, kumekuwa na madai kuwa simu za mkononi za baadhi ya abiria zilikuwa zikiita zilipopigwa siku kadhaa baada ya ripoti ya kupotea kwa ndege. Hii inaashiria kuwa popote ilipo ndege kutakuwa ni nchi kavu na eneo ambalo kuna maendeleo ya mwanadamu hoja kuu ikiwa penye mawasiliano ya simu za mkononi lazima pawe na minara ya simu na minara iyo kibiashara husimikwa kuzingatia na idadi ya watu wanaopatikana katika eneo. Hili swala mpaka sasa halijakanushwa na imeelezwa kuwa simu moja ilipokelewa na kukatwa. Kama ni kweli hiki ni kiashiria kuwa ndege haijaanguka na ipo salama. Iwapo ingekuwa imeenguka inamaana kufikia sasa ingeonekana kwa vile simu zimeita inamaana ipo eneo lenye watu na hivyo mrejesho wa ajali ungepatikana.

Jambo la nne na ambalo halijapewa kipaumbele na media nyingin hasa TV, ni kuwa katika ndege ile kulikuwa na abiria wasio wa kawaida, abiria hawa wa kipekee ni wahandisi 20, 12 kutoka taifa la Malaysia na 8 kutoka uchina. Hawa ni wataalam wa juu sana wa maswala yanayohusiana na nishati mbadala pamoja na teknolojia inayohusu mambo ya kiusalama. Wataalam hawa wanafanya kazi kule Austin, Texas kwenye kampuni inayoitwa Freescale.
Utaona kwa hapo neno usalama (defense) alijitokezi lakini ni kwa sababu mahususi, maswala ya usalama huwa hayawekwi wazi. Inawezekana kuna suala la ugunduzi mpya wa teknolojia ya usalama na yenye maslai makubwa walikuwanao. Kwa wenye kumbukumbu nzuri mwaka 1985 kuna wanataalam 17 wakijapan nao walikufa baada ya ndege yao kuanguka, jamaa hawa walikuwa na ugunduzi wa mfumo mpya wa kuendesha kompyuta (OS) uliokuwa mahiri zaidi ya ule wa Microsoft. Kawaida ugunduzi usajiliwa na muhusika kupata hatimiliki inayoitwa PATENT, asilimia zaidi ya 90% ya patent usajiliwa marekani au zinamilikiwa marekani. Ningeshauri wasomaji mfanye utafiti zaidi hapa, kunawezakuwa na mengi kwenye hili jambo.

Jambo la tano, imethibitika kuwa pamoja na kuwa ndege ilipotea kwenye radar zote za Malaysia baada ya kuvuka malango ya Malacca injini zinaonekana kuendelea kufanya kazi kwa zaidi ya masaaa matano kwa mujibu wa Boeing. Huu ni ushaidi kuwa ndege haikuanguka huko Malacca. Ndege za boieng zimewekwa kifaa maalum cha kueleza ufanisi na ufanyaji kazi wa injini za ndege, wakati ndege ikiwa angani kifaa hiki uendelea kurusha taarifa kwa satelaiti ambayo uzichukua na kuzipeleka kwenye database ya injini maintenance iliyopo makao makuu ya Boeing. Kwa bahati mbaya satelaiti huwa hazina uwezo wa kueleza eneo (position) ya kituma taarifa (transmitter) na hivyo ni ngumu kuweza kuto taarifa ya sehem ndege ilipoelekea. Uhitaji zaidi ya satelaiti tatu kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kutoa position ndivyo mfumo wa GPS unavyofanya kazi. Hii imezidi kuhififisha hoja ya ajali yaani kuanguka. Hoja ya ajali pia imeshindwa kwa kuwa nayo inazaa swali la iwaje black box ishindwe kuleta signal na tunajua teknolojia ya black box sasa imeboreshwa tangu ile ajali ya TWA Flight 800 na Air France Flight 447 zilizoangukia baharini.

Jambo la sita na jipya lililoanza alfajir ya leo ni kuwa ndege inawezekana imetekwa na maharamia na imeelekezwa bahari ya hindi. Bonyeza Missing plane: Piracy theory gains more credence. Ilianza dhana ya magaidi wa ki-Irani na sasa tunaelekea kwenye uharamia wa bahari ya hindi. Swali ni kama lengo la maharamia ni kuiangusha ndege kwanini wasifanye hivyo kwenye Bahari ya kusini ya china na waelekee bahari ya hindi? Tunajua kwenye meli wanaziteka zaidi zile za bahari ya hindi na kuzipeleka karibu na Mogadishu sababu ndiko waliko na ngome kubwa na nirahisi kuingiza na kutakatisha zile dola za ransom.

HITIMISHO:
Dalili zinaonesha kuna kuficha taarifa na kupindisha kwa makusudi taarifa za hili tukio. Kutokana na kubadilika badilika kwa maelezo na taarifa za msingi kutotolewa yawezekana kuna swala lenye maslai ju ya ndege hii, abiria wake au mizigo iliyomo ndani. Ndege za karne hii zimefungwa vifaa lukuki vya kurekodi taarifa, kuripoti taarifa, kutoa onyo na hata kuiendesha ndege kiotomatiki pale parameter za rubani zinapoonekana kuwa si sahii. Boeng 777 ni moja ya ndege zenye advanced electronics system and Avionics, kwa hiyo lazima imeacha trace sehemu. Dunia ya leo inateknolojia kubwa sana kuweza kutueleza yaliyojiri bila taabu, si kama enzi za Titanic.

Kumeanza kuwa na wasiwasi wa ndege kuwa imeshambuliwa na kutekwa kielektroniki na shirika lenye nguvu za kiteknolojia ambalo liliweza kwanza kujam signal za ndege na hivyo kupelekea kuzimwa kwa transponder, kufutika kwenye radar za kiraia na baadae za kijeshi. Teknoloji hii hipo na mara nyingi imekuwa ikifanywa na yale madege yenye antenna kama uyoga karibu na mkia, zinajulikana kama AWACS. Hizi uzipoteza signal za radar za ardhini na kuficha ndege zilizo angani zisionekane na radar ya aina yoyote. Majeshi ya marekani hutumia hizi sana kuzipoteza radar za maadui wao wakati wa mashambulizi na kuzifanya zishindwe kuona ndege zilizo angani. Mara nyingi huwa zinasindikiza fighter squadrons zinapokwenda mstari wa mbele kwa kuzipa radar support na stealth cover.

Kwa hiyo kupatikana kwa ndege hii kunaweza zalisha mzozo mkubwa sana na mlolongo wa maswali kutegemeana na wapi itakapopatikana, ikipatikana ardhini maswali yatakuwa ni mengi mno maana nchi zote zilizo jirani na ndani ya range ya uwezo wa ile ndege zina advanced radar kwa iyo zingeiona tangu inaingia kwa anga yao.

Ikipatikana baharini nako ni maswali lukuki, maana bahari ya kusini ya china inazaidi ya majeshi matatu highly advanced na kutokana na kuwa na mzozo, yanafuatilia kinachoendelea angani na majini masaa 24. Yawezekana ndio sababu ya hoja mpya ya leo asbui kuwa ndege itakuwa imetekwa na maharamia na imepelekwa bahari ya hindi. Tunafaham huko hakuna uwepo wa majeshi yenye kufanya monitoring ya maji na air space zaidi ya yale ya marekani. Kwa wanaofahamu na waliobahatika kusafir na meli kutoka Asia mpaka Africa watathibitisha hili jinsi walivyokutana na utitiri wa monitoring ya wamarekani, ukitakiwa kuji-identify (kutoa taarifa za chombo chako) kila baada ya masaa kadhaa.
Previous
Next Post »