WATU Kumi na tano (15) wamenusufika Kifo baada ya gari la abiria, walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi ya mbele na kusababisha basi hilo kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Miembeni Mkoani morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile, amesema kuwa, gari la kampuni ya Nganga yenye namba T 252 AZU aina ya Scania, lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa Alex Eliasi (49), liliacha njia na kupinduka katika eneo la Miembeni karibu na Mikese na kusababisha majeruhi ya Watu kumi na tano, Machi 31, mwaka huu, wakiwemo wanaume tisa na Wanawake sita, ambapo alisema hakuna kifo katika ajali hiyo.
Aidha alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele la upande wa kulia, hali iliyosababisha basi hilo kuyumba na kuacha njia
Amewataja majeruhi hao kuwa ni Hussein Issa (45) Msomali na mfanyabiashara wa Sumbawanga, Ignisa James (21) mkazi wa Dar es salaam, Agness Mwananza (25) Mfipa mkazi wa Dar es salaam, Christopha Kito (33) Mnyitamba na mfanyabiashara wa Dar es salaam, Agustino Kimilala (44) Mmanji na dereva wa Halamashauri ya Wilaya ya Mbarali Mbeya.
Wengine ni Mwajuma Halifa (4) Mpare, mkazi wa Kibaha Pwani, Lugano Mwamakambo (30) Mnyakusa, makazi wa Uyole Mbeya, Essau John (28) Mbena na Mwalimu wa Makambako Sekondari, Sophia Hamisi (25) kabila Mzaramo mkazi wa Dar es salaam, Abedi Athumani (48) Msambaa na mkazi wa Mbeya, Hededi Mtego (23) Mluguru, mkazi wa Morogoro, Hisia Bahati (31) mkazi wa Dar es salaam, Jane Lawa (60) Mnyakiusa mkazi wa Mbeya, Jema Mwanyakule (30) mkulima na mkazi wa Mbeya na mmoja ambaye aliridhika na hali aliyokuwa nayo na kuruhusiwa kuendelea na safari aliyekuwepo kati ya majeruhi hao.
Amesema majeruhi wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro walipolazwa ambapo baadhi ya Wagonjwa hali zao zinaendelea kuboreka huku dereva wa gari hilo akiendelea kuhojiwa na Jeshi hilo Mkoani Morogoro.
EmoticonEmoticon