Inasemekana eti huyu ndo Candy Baada ya Kufika China |
WARAKA
Ndugu Waziri Membe, Tunasikitika sana kwa haya yaliyotokea kwa sababu tumepoteza muda wetu mrefu sana kwa kuwafaidisha watu ambao wanatumia unyama kutufanyisha kazi ndugu zao ambao wengine ni dada zao wengine wadogo zao lakini wana force waitwe mama kwa ajili ya pesa zao na kutuuzisha miili kwa nguvu ili wapate wao pesa, na kutupokonya Haki zetu za msingi kama Passport ambayo hatakiwi kushika mtu ambae hausiki na Passport lakini wao wanatupokonya Passport zetu kinguvu na kuzishika wao, na mpaka sasa hivi tunasikitika hadi kuomba msaada ni kwamba tunahitaji mtusaidie kutukamatia hawa ambao wamepokonya Passport zetu na wamekimbia mpaka sasa hivi hatujui wapo wapi, kwa kuwa nyie ni mtandao wa serikali ni mkubwa tunahitaji kurudishiwa Passport zetu kwani tumepoteza muda tuna watoto wetu tumewaacha Tanzania tuna familia zetu tumekuja kutafuta maisha lakini tulichotegemea sicho tulichokikuta ila tunaomba msaada tupate Passport zetu zirudi mikononi mwetu, kwasababu ajira zipo nyingi China hata kama tutaendelea kufanya kazi huku basi iwe rahisi kwa kuwa tutakua na Passport, China kuna kazi nyingi kama za kuuza Mama Ntilie za waghana au kuhudumia za wachinalakini wao wametulazimisha kufanya kazi yao ya Kujiuza, sisi hatupo tayari kufanya kazi hii ya Uharamu tutatafuta ajira nyingine kwa kutumia mikono yetu sisi tunapingana na umaskini na tunatambua ya kwamba vijana ndio nguvu ya taifa, tunaomba msaada mheshimiwa waziri Membe, hatukuja kwa lengo la biashara ya Ngono labda hao wa mama waliotutangulia hiyo ndio kazi yao kama huyo Mama anayeitwa Havintishi anayeuza mama ntilie katika mji wa Ghuang Zhou jengo moja linaitwa Tinshuu ghorofa ya Tisa wapo wengi sana ukienda katika ile ofisi utakuta wadada wengi sana. MWISHOOOOO
Mwanadada Candy kwa huku Tanzania yeye ni mkazi wa jijini Mbeya kwa Kina ndaga fijooooo, mwezi wa December mwaka jana 2013 alikutana na Dada mmoja huko Mbeya akamwambia kama yuko tayari amchukue waende China kwani kuna Mchongo wa Kazi za Umama Ntilie basi Candy pasi na kujua kuwa anaingia chaka akajikusanya na kuwaaga nduguze safari Ikaanza, kufika China Candy akafanyiwa bonge la shopping mwanadada akapendeza sanaaaaaaaaaaaaaaa
Ila baada ya Ile shopping ni maumivu mpaka leo kwani amenyang'anywa Passport na anauzwa mwili wake kwa kulala na wanaume na pesa ikiingia anaichukua tajiri yake.
Skiza Sauti ya Mwanadada huyo kama alivyotiririka kwenye You Heard ya XXL/Cloudsfm - See more at: http://www.makorokocho.co/2014/03/you-heard-waraka-wa-mtanzania.html#sthash.AderZZoS.FWiL8fdS.dpuf
SOURCE GAZETI LA MAKOROKOCHO
EmoticonEmoticon