RAIA wa Kenya, Joshua Likumbi (45), amefariki dunia katika ajali ya basi la Kampuni ya Hood linalofanya safari zake kati ya Arusha na Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea jana baada ya gari hilo lililokuwa likielekea Mbeya kupasuka tairi la mbele lililosababisha gari hilo kuacha njia na kupinduka huku abiria wengine 16 wakijeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Robert Boaz, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo saa 3 asubuhi katika Kijiji cha Kiverenge, barabara ya Mwanga-Same likihusisha gari lenye namba za usajili T 488 AXV aina ya Scania.
EmoticonEmoticon