TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.02.2014.
Ø
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
BARABARANI WILAYA YA MBOZI.
Ø
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI MICHE 30.
Ø
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI .
Ø
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LA MSHIKILIA MTU MMOJA KWA
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO].
Ø
JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA/BUNDUKI TANO [05] AINA
YA GOBOLE BAADA YA KUTELEKEZWA/SALIMISHWA
NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI
WILAYA YA MBOZI.
MTU
MMOJA MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ISACK ZULU @ MGODE [21] MKAZI WA KIJIJI CHA ILEMBO WILAYA YA MBOZI ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI IT
1438 AINA YA TOYOTA ALLION LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ELIA MWANDOLWA [33]. TUKIO HILO
LIMETOKEA TAREHE 18.02.2014 MAJIRA
YA SAA 13:30HRS MCHANA ENEO LA VWAWA BARABARA KUU YA MBEYA /TUNDUMA. AWALI GARI HILO LILIGONGA GARI JINGINE LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.957 CRV AINA YA TOYOTA RAV 4 LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA THOMAS MWILENGA AMBAYE HATA
HIVYO HAKUSIMAMA BAADA YA KUGONGWA. CHANZO
CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA GARI IT 1438. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI YA WILAYA YA MBOZI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA
KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT
MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI WENGINE WA
BARABARA KUWA MAKINI NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA
NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMSHIKILIA
MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI MICHE 30.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA FREDRICK SIMBEYE [41] MKAZI WA KIJIJI CHA ILULU WILAYANI ILEJE MKOA WA MBEYA BAADA YA
KUKAMATWA AKIWA NA BHANGI MICHE
30 ALIYOKUWA AMEPANDA KATIKATI YA
SHAMBA LAKE LA MAHINDI. MTU HUYO ALIKAMATWA TAREHE 18.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS
MCHANA ENEO HILO KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. MTUHUMIWA NI
MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOLIMA
ZAO HARAMU LA BHANGI AU KUUZA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA
ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMSHIKILIA
MTU MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA ANTHONY ADAMU [34] MKAZI WA KIJIJI CHA UJERUMANI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA
MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA ANAMILIKI
SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI ALIYOKUWA AMEPANDA KWA KUCHANGANYA
NA ZAO LA MAHINDI. MTU HUYO ALIKAMATWA TAREHE 18.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:30HRS
ASUBUHI ENEO HILO KUFUATIA MSAKO
ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA
BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOLIMA MASHAMBA YA BHANGI AU KUUZA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMSHIKILIA
MTU MMOJA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] .
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
ESTERIA ANDALWISYE [72] MKAZI WA MTAA WA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MOJA
[01] . MTU HUYO ALIKAMATWA TAREHE 18.02.2014
MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI ENEO HILO KUFUATIA MSAKO
ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. MTUHUMIWA HUYO NI MTENGENEZAJI/MTUMIAJI NA MUUZAJI
WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA TANO
[05] AINA YA GOBOLE BAADA YA KUTELEKEZWA/KUSALIMISHWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKAMATA SILAHA
/BUNDUKI TANO [05]AINA YA GOBOLE AMBAZO ZIMETELEKEZWA/SALIMISHWA NA WATU
WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 18.02.2014
MAJIRA YA SAA 07:45HRS ASUBUHI KATIKA
KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA WAKATI ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA
DORIA/MSAKO. SILAHA HIZO AMBAZO ZIMEHIFADHIWA POLISI ZILIKUWA ZINAMILIKIWA NA
WATU HAO KINYUME CHA SHERIA. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KUFUATA TARATIBU KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA BILA KIBALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO IKIWA NI PAMOJA NA MTU/WATU WANAOMILIKI
SILAHA KIHALALI LAKINI WANAZITUMIA KATIKA MATUKIO YA UHALIFU AZITOE ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI
YAO ZICHUKULIWE.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon