TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.02.2014.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

 


RPC.                                                                                                Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                              Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                          S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                   MBEYA.
E-mail:-  rp.cmbeya@tpf.go.tz                                                                      




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.02.2014.




·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI RUNGWE.





·         MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.





·         MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.





·         MTU MMOJA ANASHIKILIWA NAJESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA SILAHA [RIFFLE] BILA KIBALI.





MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI RUNGWE.

MTU MMOJA ALIFAHAMIKA KWA JINA LA SIFA MPOLOGWE (33) MKAZI WA IGOGWE ALIUAWA KWA KUPIGWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA KATIKA KIJIJI CHA NTOKELA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA  YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.



MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU KATIKA SHULE YA SEKONDARI NALYELE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA USHINDI MWAEMBE (17) MKAZI WA MAHENJE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AINA YA CANTER LILILOKUWA LIKINDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENJE  WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA  YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. PIA ANAWATAKA MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI NI HATARI NA UNAUA.





 



MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARIA AUGEN (33) MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA 14:15HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAJENGO  WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HIYO KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.




MTU MMOJA ANASHIKILIWA NAJESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA SILAHA [RIFFLE] BILA KIBALI.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAMECK BUKWIMBA (44) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA RIFFLE YENYE NAMBA K-79614 NA RISASI MBILI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA 17:50HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA AKIWA AMEIFUNGUA SILAHA HIYO VIPANDE VIPANDE NA KUIFICHA KATIKA MFUKO WA SANDARUSI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYIKA IKIWA NI PAMOJA NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA[BILA KIBALI] NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA KUMILIKI SILAHA KIHALALI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYOVYOTE ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.



Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »