SARAH SHILLA NI 'FASHION MODEL' ANAYEWIKA KWENYE UIMBAJI, AITIKISA INDIA

 



Sarah Shilla akitoka kihindi stejini, vazi mojawapo lililomtoa kimasomaso.


Pamoja na kuwa miongoni mwa wamibaji ambao wanagusa mioyo ya wananchi, hasahasa kutonaka na wimbo wake wa 'Natamani', muimbaji Sarah Shilla pia hujihusisha na uanamitindo. Hilo, limempa kuwa mwanadada pekee aliyewapiku wazawa nchini India, na kuchukua dili Italian Wear, na Indian Brand. Na KWA TAARIFA YAKO, analipwa kwa kuvaa nguo za makampuni hayo.

Kama ambavyo mtu anaweza kuwa na vipaji mbalimbali, Sarah, ametokea kuguswa na uanamitindo, na hili hajaanza nalo mbali, ila ni hapo hapo chuoni, ambapo siku moja kulikuwa michuano ya kiuanamitindo, ambapo vyuo mbalimbali vilishiriki, yeye pia akishiriki. Na mwisho wa siku, chuo chake kikaibuka na ushindi, kuanzaia hapo, akaamua akazane na uanamitindo, baada ya kuvutiwa nao - kubwa likiwa ni utanashati, na muonekano.

Baada ya kuanza kufanya mazoez kwa takriban miezi mitatu, kwa kufanya jogging, na kwenda gym, kutabasamu, mwendo wakati wa kutembea, na hata vipimo sahihi vya 'make-up', Sarah akajitosa kushiriki kwenye mashindano ya kutafuta models' ambao watakuwa mabalozi wa kampuni za mavazi nchini humo, ambapo washiriki takriban 30 walijitokeza, huku idadi ya wanaohitajika ikiwa ni 12 tu, ambapo nusu yake ikiwa ni wanaume, na nusu nyingine ikiwa ni wakinadada. Na kati ya hao 6 kwa pande zote, hapo ndipo mtu mmoja mmoja apatikane kwa kila upande.

KWA TAARIFA YAKO, Kati ya washiriki wote, ambao wengi wao wakiwa Wahindi, na mmoja kutoka Nepal, Sarah alikuwa Mwafrika pekee akiwa pamoja na Mganda. Licha ya kukosewa walipopambwa (make-up), jambo lililowapelekea yeye na Mganda kupambana wenyewe, Sarah Shilla aliibuka mshindi, akiwaduwaza wazawa.

Sio make-up tu ambazo zilikuwa zikitazamwa, bali pia nguo, pozi, tabasamu, na hata style ya nywele zilikuwa chachu ya ushindi wa Sarah, kwenye shindano hilo la wazi lililofanyika kwenye shopping mall ya Westand, na kushuhudiwa na ya watu kwenye jengo lenye takriban ghorofa 8.

Kwa ushindi huo, Sarah anachukua mshiko na nguo kadhaa ambazo anazivaa kuwakilisha nembo ya makampuni waliyoingia nayo mkataba, ambao unadumu kwa mwaka mmoja, ikiwemo evening wears, sarees, jeans, na tshirts.


Sarah (kushoto) akiwa amekabidhiwa mkoba wa zawadi ya mshindi namba moja, hapo bado kitita.
Pamoja na mkataba wake kuwa wa mwaka mmoja, KWA TAARIFA YAKO, Sarah hatoumaliza mkataba,   na badala yake atarejea Tanzania baada ya kumaliza masomo yale mnamo mwezi Mei, na licha ya kufanya hivyo, mkakati wa modelling bado utaendelezwa kwa hapa nchini, ni kwa mfumo gani, endelea kukaa chonjo utafahamishwa kupitia hapahapa GK, lakini pia KWA TAARIFA YAKO, designer wa nguo na costumes kwa video zake, ni yeye mwenyewe, kwa utaalamu alionao kwenye modeling, hana haja ya kutafuta mtaalamu wa nje.
Previous
Next Post »