Mapigano makali yanaendelea katika eneo la kwa mzee Juma kata ya Mbezi Juu Dar es salaam


Hili ni kundi la vijana waendesha bodaboda wakienda mtoni kumwokoa mwenzao ambaye wanadai ametekwa na wahuni wanaojificha mtoni na kukaba watu, mpaka sasa boda boda aliyetekwa yupo mwananyamala hospital na mmoja wa vijana wanaoaaminika kwamba ni vibakaba ameshauawa
Kuna mapigano makali eneo la kwa mzee Juma Kata ya Mbezi juu.
Habari zaidi zionasema kwamba Waendesha Bodaboda hao wanaendelea kupambana kwa kutumia silaha za jadi dhidi ya vijana wanaosemekana aidha ni vibaka au wameiba pikipiki ya mwenzao.
Hali ni mbaya majeruhi ni wengi na inasemekana kuna vifo vimetokea.
chanzo kapinga blog
Previous
Next Post »