Couple ya inayoundwa na rapper mwenye mashabiki wengi na ‘temper’ ya aina yake, Kanye West na mrembo Kim Kardashian, inatarajia kufunga pingu za maisha May mwaka huu tofauti na ilivyoripotiwa awali kuwa ingekuwa July. Us Weekly imeripoti.
Sehemu litakapofanyika tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wao iliwahi kutajwa na Kim Kardashian katika show ya ‘Jimmy Kimmel Live!’, “I’m not telling where or the date, but I think it’s kind of obvious it’s Paris.”
Hivi karibuni wawili hao walikuwa jijini Paris ambapo waliwaalika watu kadhaa kwa ajili ya chakula cha usiku, na kati yao walikuwemo watu wanaofanya nao biashara. Ripoti kutoka jijini Paris zilidai kuwa wawili hao walikuwa wanatafuta sehemu watakayofungia ndoa yao.
Katika tukio hilo linalotarajiwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa, inasemekana Kanye West atatumia zaidi ya $ milioni 30 kuwasafirisha wageni waalikwa hadi eneo tukio na kuwarudisha maskani yao.
Ingawa wawili hao walimficha sana mtoto wao asikutane na camera za paparazzi hapo awali, mtoto huyo anatarajiwa kuwa na jukumu la aina yake na kuonekana zaidi siku hiyo ambapo imesemekana Kanye West atatumia pesa nyingi kuhakikisha linaoneshwa kwenye vituo vya runinga.
EmoticonEmoticon