WILAYA YA RUNGWE – AJALI
YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
[ASKARI] NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 05.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:50HRS HUKO ENEO LA MBEYA ONE, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE,
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. ASKARI EX WP 1601
S/SGT BENADETHA, MIAKA 52, MCHAGA,
ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI TUKUYU WILAYA YA RUNGWE, AKIWA KAZINI ENEO HILO ALIGONGWA NA
GARI T.613 BUM AINA YA TOYOTA
CARINA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST S/O MATHAYO NDOA, MMAKUA, MIAKA 35, MKAZI WA KYELA NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI
TUKUYU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI NI HATARI NA UNAUA.
Signed by:
[AHMED. Z. MSANGI –
SACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon