Mwili
wa aliekua Waziri wa fedha na Uchumi Dr. William Mgimwa unatarajiwa kuwasili
Dar es salaam Tanzania kesho Jumamosi Jan 4 2014 ukitokea Afrika Kusini kwenye
hospitali aliyokua kalazwa.
Mwenyekiti
wa kamati ya kitaifa ya mazishi ambae ni Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu
sera uratibu na bunge William Lukuvi amesema baada ya kuwasili Jumamosi
hiyohiyo saa tano asubuhi ataagwa kwenye viwanja vya Karimjee Dar es salaam
kabla ya kusafirishwa kuelekea Magunga Iringa kwa maziko January 6.
EmoticonEmoticon