Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera.
Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiiugua Saratani kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39. Mungu ailaze roho ya Ann mahala pema peponi.
EmoticonEmoticon