Na:
Meshack Maganga
Wakati tunaelekea
kwenye kipindi cha kuanza kupanda na kuotesha miti mipya ya msimu wa 2014- 15
ambao huanza rasimi mwezi wa 12 wa kila mwaka, watu wengi sana walitutumia
email na kutupigia simu, kulizia
taratibu za kupata maeneo ya
kupata mashamba, na wale wenye mashamba walitupgia kuulizia namna ya
kupata miche ama kununua mashamba yenye
miti zaidi ya yale waliyonayo kwa sasa. Makala hii fupi inafafanua kwa undani
zaidi, hii ni kwa faida ya watu wengine.
Unaweza kununua
mashamba yenye miti tayari kwa mchanganuo ufuatao
Miti pamoja na ardhi: Miti ya mwaka mmoja . (Bei zinatofautiana kutokana na ‘location’ yalipo mashamba husika). Mashamba ambayo hayana kitu. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni shilingi laki mbili kwa ekari moja
Miti pamoja na ardhi: Miti ya mwaka mmoja . (Bei zinatofautiana kutokana na ‘location’ yalipo mashamba husika). Mashamba ambayo hayana kitu. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni shilingi laki mbili kwa ekari moja
Hata hivyo unaweza kupata mashamba haya yenye miti kwa bei za chini
zaidi ya hizo kutegemea na wenyeji unaokutana nao pamoja na maeneo
husika na idadi ya ekari unazonunua.
Ukinunua shamba tupu itakugharimu wastani wa shilingi laki tatu hadi
nne katika kuandaa shamba hadi kupanda. Kwa ushauri wetu tunakushauri kama ukiweza ni vema kutafuta mashamba yenye miti tayari, ununue. HII itakusaidia kuepusha usumbufu wa kuandaa na kupanda hadi ishike ardhini. Ukishanunua shamba iwe ni kutoka kwetu ama kwa wenyeji, kunakuwa na ‘documents’ ambazo zinatolewa na serikali ya kijiji husika kwa idhini ya kamati ya ardhi ya kijiji.
Kwa upande wetu
(ikitokea unanunua kutoka plots za kampuni) mara zote management fee
tunaijumlisha katika bei ya manunuzi. Kitu ambacho utaendelea kufanya ni
kugharimia uhudumiaji wa shamba ambao una shughuli kubwa mbili; 1)
Kuproon-wastani wa shilingi laki moja kwa ekari na inafanyika mara mbili hadi
tatu kuanzia kupanda hadi kuvuna. 2) Kutengeneza njia kuzunguka shamba na inafanyika
kila mwaka na ni wastani wa shilingi elfu sitini kwa ekari moja.
Miti ipo ya aina
tofauti. Kwa hapa Iringa kuna miti ya aina mbili inayostawi; ya (nguzo na mbao)
iitwayo milingoti naya (karatasi na mbao) iitwayo Pines. Hii ya milingoti
inachukua muda mfupi zaidi kukua (wastani wa miaka mitano hadi saba ikiwa ni
kwa matumizi ya nguzo na mirunda hutumia miaka miwili hadi mitatu) na pines
ambayo ni maalumu kwa ajili ya mbao na kutengenezea karatasi inachukua miaka 7
hadi kumi mpaka kuvunwa.
Ekari moja inachukua
miche 500 mpaka 600 na ‘survival rate’ ya aina zote mbili nilizokutajia ipo
asilimia 80%.
Uvunaji upo wa aina
mbili. Unaweza kuamua kuuza miti kama miti (yaani magogo) ambapo kwa miti hii
ya nguzo kwa mti mmoja uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia 20,000 na kuendelea.
Kwa upande wa miti ya mbao na karatasi mti uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia
20,000 na kuendelea (ingawa hii pia inaamuliwa na ‘location’ ya shamba. Shamba
linapokuwa mahali kusikofikika bei ni ndogo zaidi). Namna ya pili ya uvunaji ni
kuvuna mwenyewe kwa maana ya ama kupasua mbao au kutengeneza nguzo za umeme za
kuuza. Katika hii ‘option’ ya pili ya uvunaji inakulazimu uwe katika biashara
kamili ya mbao kwa sababu utahitaji mashine, leseni, vibali na taratibu
nyingine.
Hadi sasa tunavyoongea,
hali ya soko la mbao na nguzo/mirunda liko juu sana na demand ni kubwa kuliko
supply. Nadhani unatambua kuwa mahitaji ya bidhaa za miti yameongezeka kwa kasi
sana miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika na
wataalamu wakiwemo SUA wanatueleza kuwa soko la bidhaa za misitu (mbao, nguzo
n.k) litaendelea kupanda bila kushuka kwa miaka 25 ijayo kuanzia mwaka 2010.
Kama wawekezaji tunakuwa positive katika hilo ijapokuwa hatuachi kuweka
tahadhari ya risks (ikiwemo market changes) kama ambavyo ni kawaida kwa
biashara yeyote duniani
Ninaamini nimekupa ufafanuzi mzuri na mahali popote ambapo utakuwa hujapaelewa ama unahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuwasiliana nami. Ni furaha yangu ukisaidika na kufanikiwa.
Ninaamini nimekupa ufafanuzi mzuri na mahali popote ambapo utakuwa hujapaelewa ama unahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuwasiliana nami. Ni furaha yangu ukisaidika na kufanikiwa.
Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara katika
makala zangu; ni kwamba muda wa kulalamika lalamika umekwisha. Mazoea na
utamaduni wa watanzania wengi kudhani kwamba tunaonewa wakati wote
haujatusaidia mpaka hapa kwa jinsi hii hakuna sababu ya kuendelea nao.
Mtindo wa kuishi maisha ya kutaka kuhurumiwa
yanatupotezea muda wenye thamani. Tumekuwa tukilalamika kuwa wageni (wanaokuja
kwa jina la wawekezaji) wanatupora ardhi; lakini tusichokitafakari ni hiki,
“Mimi kama mtanzania kwa nafsi yangu na kwa uwezo wangu nimefanya nini cha
maana katika ardhi ninayoweza kuipata hapa nchini ama ninayomiliki?”.
meshackmaganga@gmail.com
0767 48 66 36 ama 0713 48 66 36.
Website
http://freshfarm.co.tz/
EmoticonEmoticon