MSANII wa maarufu wa filamu Tanzania, Hisani Muya ‘Tino’, amesema filamu za Bongo haziwezi kuuza bila kuwa na wasichana warembo.
Akizungumza na mtandao wa Bongo 5 jijini Dar es Salaam jana, Tino alisema hakuna atakayenunua filamu hizo na huenda waandaaji wakaishia kuangalia tu nyumbani na familia zao.
Alisema, wasichana warembo ni ‘chambo’ kinachowavutia wanunuzi wa filamu za Tanzania, ujuzi na uigizaji au kipaji si sababu kwao.
Aidha, alisema warembo hao pamoja na kuzifanya filamu zivutie, pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume na wanaipenda kazi yao.
“Bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako, haitauza kwa sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,” alisema Tino.
Tino alienda mbali na kuwataja waigizaji wa kike, ambao wanaweza kuuza filamu zake kuwa ni pamoja na Wema Sepetu, Irene Uwoya, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jaqueline Wolper, Batuli, Monalisa, Dianarose na wengine.
EmoticonEmoticon